GET /api/v0.1/hansard/entries/182720/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 182720,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/182720/?format=api",
"text_counter": 550,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kambi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 39,
"legal_name": "Samuel Kazungu Kambi",
"slug": "samuel-kambi"
},
"content": "Asante sana Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ambayo iko mbele yetu. Swala la usalama ni muhimu sana katika nchi hii; ni swala ambalo ni nyeti mno. Ukiangalia yale ambayo yanatukia kila siku na sisi viongozi tunaangalia na hatuwezi kupata suluhisho, basi inaonyesha tuna matatizo. Kuna shida ya vijana. Utapata kwamba wale ambao hufanya uhalifu ni vijana. Shida kubwa ambayo iko ni ukosefu wa ajira. Sisi viongozi inafaa tukae na tupate suluhu, ili vijana ambao hawana kazi, na wanarandaranda, wapate ajira. Bw. Naibu Spika, tatizo lingine ambalo lipo, hata kama tukiwa na tume, kama hatutakubali, kama viongozi, kwamba kuna matatizo na hatuna njia ya kuyatatua, basi tutakuwa tunaongea kitu ambacho ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Ukiangalia watu ambao tumewapatia kazi ya kutulinda, wana shida. Ukiwauliza kwa nini October 23, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 3017 kuna uhalifu mwingi, wao hawatakuambia. Tunashukuru kuwa tuna Kamishina wa Polisi ambaye alitoka kwa jeshi, lakini haelewi ile system ya polisi. Hata akijaribu, kuna wale ambao wako chini yake, na wanaona kweli anajaribu lakini haelewi kazi hiyo. Sisi kama viongozi tungependelea tuwe na Kamishina wa Polisi ambaye amehudumia katika viwango vya chini, na kupandishwa vyeo, hadi kiwango cha juu; asiwe ametoka mahali pengine. Hivyo tutakuwa tunaanza kuyaingilia hayo matatizo. Vile vile, motisha ya wafanyakazi ambao tumewaamini kutulinda, ama kulinda usalama, iko chini kwa sababu mishahara yao iko chini. Hawawezi kuzichunga familia zao vizuri. Utakuta kwamba mkuu wa kituo cha polisi, kwa mfano cha Kaloleni, ana watoto kumi walio shuleni, na badala ya kutuchunga, ataanza kutafuta hongo kwa sababu mshahara hautoshi. Haya ni matatizo ambayo inafaa tuyaangalie. Inafaa sisi viongozi tujitokeze ili tuweze kusaidia, kwa sababu tuna matatizo na uhalifu umezidi. Kila wiki, mahali popote ni lazima watu wanauawa. Ukiangalia wakati mwingine ni sisi viongozi tunaowaambia watu juu ya kabila fulani. Ningependa sisi viongozi tuwe kwenye msitari wa kwanza wa kuwaambia wananchi kwamba hii ni nchi yetu sisi sote, na kuna umuhimu wa kuishi kama ndugu na si kusema kwamba yule ni Mjaluo, au kuliambia kabila fulani liende likapige kabila lingine. Kwa hivyo, ikiwa matamshi yetu hayatakuwa ya kuonyesha kwamba sisi ni watu wa nchi moja, ama ni ndugu tutaendelea kuwa na hili tatizo la ukosefu wa usalama. Ningependa---"
}