GET /api/v0.1/hansard/entries/182962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 182962,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/182962/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Asante, Bi Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchangia Hoja hii kwa lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa. Juzi, baada ya Rais kuhutubia wananchi na kutoa hotuba yake kwa kimombo, kulikuwa na malalamishi kidogo aliposimama na kukosa kuzungumzia wananchi kwa Kiswahili. Inanibidi kujikumbusha kidogo lugha yetu ya taifa. Tukianza kusema, kwanza muundo na uundaji wa wilaya na mikoa si jambo la kisiasa, bali ni haki ya Wakenya. Ni haki yao kupitia Katiba. Nia ya kuunda wilaya mpya ni kurahisisha utoaji wa huduma kwa umma. Mkoa ninakotoka unaanza kutoka Mombasa mpaka Nairobi, halafu unasonga na kupakana na Bonde la Ufa na Mkoa wa Kati. Inabidi watu wa Kibwezi kuenda mpaka Embu kupata huduma kutoka Mkuu wa Mkoa. Haya ni mateso bila chuki. Kwa hivyo, tusije tukaingiza siasa kwenye jambo hili kwa sababu mara nyingi Rais wetu wametangaza kubuniwa wa wilaya na kata mpya mbele ya umati wa watu au katika matembezi yao ya siasa. Kubuniwa kwa wilaya hizo kulitokana na wananchi wenyewe kwa sababu wao ndio waliuliza. Baada ya kupata wilaya hizo, wale ambao hawakuuliza wameigeuza kuwa jambo la kisiasa. Kwa hali ya uhakika na kweli, wilaya inapoundwa, inahakikisha kuwa October 22, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 2907 wananchi wanapata huduma na haki yao. Tunapozungumza mambo haya, tunafaa kuyatenga mbali na siasa na tuseme kwamba sio tu wilaya ambazo zimebuniwa. Wilaya yangu sasa ni mpya. Ina umri wa miaka mitatu na watu 325,000. Hivi sasa, nina wilaya ambayo ina watu 75,000 au 120,000. Huyu mkuu wa wilaya pekee anatakikana awatumikie watu wale 325,000 kadiri na kulingana na yule mtu anayewatumikia watu 175. Ili watu wetu wapate huduma bora, hii ndio sababu tumeyaweka masingizio haya katika ugawaji wa rasilmali zetu. Ni lazima haki ipatikane kwa watu walio wengi. Jana, tumeona kwamba Wizara zinatoa makadirio yao ya hela. Ningependa makadirio yatakayowasilishwa hapa hapa yaende sambamba na huduma kwa watu wetu. Ninaona ya kwamba masafa yangu ya kutembea na mwendo wangu inaelekea kukosa nguvu ya kusimama hapa na kuzungumza kwa sababu tumezungumzia na tunapitisha Hoja hii. Baada ya kupitisha Hoja hizi zinakwama pale pale; hazitekelezwi. Kama Bunge hili ni Bunge la heshima na hapa ndio pana utungaji wa sheria ambazo tunatumia kuongoza nchi hii, tunataka jambo lolote tunalopitisha hapa litekelezwe mara moja. Tusiongee tu, kisha tukimaliza kuongea, mambo haya yanakwama pale pale. Tumekuwa wazungumzaji wazuri sana. Tunapendeza sana kwa lugha zetu. Tuna matamshi ya kupendeza sana. Mwisho wa mambo haya yote ni kitu gani kinachopatikana? Tumeimba hapa mara nyingi wimbo wa rasilmali kugawanywa ipasavyo kulingana na jinsi nchi ilivyo. Tutayafanya mazungumzo haya mpaka lini? Wakenya wanastahili kupatiwa mikoa, wilaya, na kata."
}