HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 184954,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/184954/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kutuny",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "Bi. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa fursa hii. Kwanza, ningependa kumshukuru Bw. Mututho kwa kuleta Hoja hii, ambayo imekuwa donda ndugu sana katika Taifa la Kenya. Wakenya wengi walijitolea ima fa ima kwa miaka mingi, ili kuleta ukombozi na Uhuru katika Taifa la Kenya. Wengi wao walipoteza maisha yao na wengi wakapoteza makao katika harakati za kuleta ukombozi katika Taifa la Kenya. Wabeberu walikuwa 2556 PARLIAMENTARY DEBATES October 8, 2008 wamelimiliki Bara la Africa na Taifa la Kenya kwa ujumla. Lakini Wakenya ambao walikuwa na maono waliweza kujitolea kwa namna yoyote ile, ili kuweza kulikomboa Taifa hili. Lakini masikitiko ni kwamba wale ambao walileta Uhuru na kutupatia mchanga na ardhi ambayo ina rutuba katika Taifa la Kenya, walikufa katika ufukara. Kwa sasa, mbegu ya ufukara wao inachipuka. Katika Taifa la Kenya, kuna vikundi tofauti tofauti. Genge la majambazi. Nikitaja vikundi vichache, kuna genge kama la Mungiki na genge la Sungu Sungu . Hayo ni matatizo ambayo tuko nayo na ukifuata kwa undani, utagundua kwamba wale ni wana wa wale watu ambao waliwania na kupambana na ubeberu ili kutupatia nafasi ya uongozi ambao tunao sasa. Lakini wachache ambao walikuja kutawala Taifa hili hawakuona umuhimu wa kuweza kuwatafuta wale watu waliowania kutupatia Uhuru katika Taifa la Kenya. Kukawa na mabwenyenye wachache katika Taifa la Kenya, wakanyakua kila kitu na ikawa mwenye nguvu mpishe. Ikawa tangu lini nguruwe akapatikana kwenye taka la simba? Walifutwa na wakasukumwa kando. Sasa tunasema hapa Bungeni kwamba wakati umefika kwetu sisi, kama taifa la Kenya, kuwanyooshea mkono wa shukrani wale waliojitolea kutupatia nafasi ya kujitawala. Hatua ya kwanza ni kubuni mikakati itakayotuwezesha kuhakikisha kwamba Hoja hii itakapotekelezwa, tutaweza kuwatambua wale watu walioweza kuwania nafasi ya Wakenya kujitawala ili tusije tukawa na watu watakaosema: \"Sisi tuliwania haki ya Wakenya\", lakini ukweli ni kwamba wao ni mbwamwitu waliovalia ngozi ya kondoo. Bi. Naibu Spika wa Muda, miaka michache iliyopita, watu fulani walienda Uhabeshi na kutuletea mtu mmoja mjanja aliyedhaniwa kuwa Jenerali Mathenge. Ukweli ni kwamba mtu huyo hakuwa miongoni mwa wanaharakati wa Mau Mau ambao walitutetea mpaka tukapata Uhuru. Kwa hivyo, tutakapoipitisha Hoja hii, ni lazima kuweko na mipango kamili ya kuwatambua wale waliopigania Uhuru wetu na kuangamiza ubeberu katika nchi ya Kenya. Pili, familia za wapiganiaji Uhuru ambazo ziko katika taifa hili ni lazima zishughulikiwe kwa kina. Tatu, tuna vyuo vingi katika taifa la Kenya. Kuna baadhi ya viongozi ambao walivipa majina yao vyuo zaidi ya 100. Tunataka baadhi ya vyuo hivyo katika kila mkoa vibadilishwe majina kupewa majina ya mashujaa walijitolea kupigania Uhuru wa nchi hii. Sisi kama wabunge kutoka Bonde la Ufa, tuna mpango wa kuleta Hoja Bungeni ili kubadilisha jina la Moi Unversity, Eldoret, liwe \"Koitalel University\", ili kuwatambua na kuwapatia heshima wale watu ambao walitetea haki ya Wakenya. Nikimalizia, ninasema kwamba tunataka tushirikiane sisi sote. Ninashukuru kwa sababu Hoja hii imefanyiwa marekebisho. Nilikuwa na wasi wasi kidogo pale Hoja hii ilipozungumzia juu ya wapiganiaji Uhuru wa Mau Mau pekee yao. Kule Mombasa, kulikuweko na vita. Kinjeketile alikuwa kule akitetea haki ya Wakenya. Vile vile, katika sehemu ya mpaka wa Kenya na Tanzania, kulikuweko na vita. Kinjeketile aliongoza vita hivyo kutoka sehemu ya pwani ya Kenya hadi kule Tanzania. Nguvu zake zilifika kote katika taifa la Kenya. Hapa Nairobi, kulikuweko na vita vilivyoongozwa na Wakenya. Kule Nyanza, kulikuweko na wakombozi. Katika sehemu zote katika taifa la Kenya, kulikuwepo na watu waliojitolea. Ndiyo tunashukuru kwa sababu ya marekebisho yaliyofanyiwa Hoja hii, ambayo yanaelekea kuwajumuisha Wakenya wote waliojitolea kuhakisha kwamba mbeberu aliondoka kutoka taifa la Kenya. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}