GET /api/v0.1/hansard/entries/184966/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 184966,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/184966/?format=api",
    "text_counter": 248,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mungatana",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi ili nami nichangie Hoja hii. Ningependa kumshukuru Bw. Mututho kwa kuleta Hoja hii Bungeni. Ametupatia nafasi ya kuweza kuzungumzia mambo muhimu kuhusu maisha yetu sisi Wakenya na hasa kuhusu historia yetu. Sote tunakubaliana kwamba ni lazima kitu kifanywe kwa ajili ya kuwakumbuka waliopigania Uhuru. Ninakubaliana na wale ambao wamependekeza mabadiliko kwa Hoja hii. Wamesema kwamba tusiwaangalie tu mashujaa wa Mau Mau bali pia tuwaangalie wapiganiaji Uhuru wote nchini. Sisi kutoka kule Mkoa wa Pwani tunamkumbuka kiongozi mashuhuri Mekatilili wa Menza ambaye alichangia pakubwa upiganiaji Uhuru kule Mkoa wa Pwani. Wapo viongozi wengine waliotajwa pia. Je, taabu imekuwa wapi? Ingawaje sisi Wabunge tunakubaliana tukiwa humu Bungeni ama kule nje kwa wananchi, tungependa kujua taabu imetokea wapi. Taabu iliyoko Kenya - si Kenya pekee yake -ni kwamba mtu ambaye amevalia suti, amefunga tai, amevalia saa na amevipiga viatu vyake rangi, akija ofisini, yeye hupewa nafasi ya kuongea na husikizwa. Lakini akija mtu amevalia 2564 PARLIAMENTARY DEBATES October 8, 2008 shuka na hakuchana nywele ama amevalia shati lililopasuka, yeye hutengwa. Askari pale ofisini hawampi nafasi ya kuingia ndani ile azungumze mambo yake. Tabia hii ya kunyanyasa maskini haikuanza leo. Ilianzishwa na sera za mkoloni. Mkoloni alimchagua mtoto wa chifu kisha akampleka shule. Alimfunza kupiga rangi viatu na akampa kaptula, suruali na nguo zingine. Mtoto huyo aliposoma, alipelekwa ulaya kwa masomo zaidi. Aliporudi, huyo ndiye mkoloni alitaka kuona. Mau Mau hawakuwa na hata kichana. Waliishi msituni na watoto wao walipata taabu. Dkt. Kilemi Mwiria aliniambia kuwa yeye alizaliwa katika"
}