GET /api/v0.1/hansard/entries/184968/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 184968,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/184968/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mungatana",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
"speaker": {
"id": 185,
"legal_name": "Danson Buya Mungatana",
"slug": "danson-mungatana"
},
"content": ". Wazee wake hawakupatiwa nafasi kusema, \"Sisi tulikuwa na taabu. Tumeng'ang'ania mambo haya.\" Marais waliokuwako hawakutaka kuwaona watu hawa kwa sababu walikuwa na nywele ndefu na walikuwa wamejitanda shuka. Hawakuweza kupatiwa nafasi na Serikali kama alivyopewa mtu wa kawaida. Serikali ilikuwa ni ya mzungu tu. Kilichofanyika ni kwamba mzungu kawa mweusi. Mzungu ni yuyo huyo aliyepewa kaptula na kupelekwa ulaya. Ni yuyo huyo aliyerudi na kushika mamlaka. Mau Mau pamoja na wapiganiaji uhuru wengine waliachwa nje kwa sababu hawakuwa safi. Akili hii ya kuwanyanyasa maskini tumeibeba kutoka enzi za Marais wetu, Mzee Kenyatta na Moi. Mpaka leo tungali na akili hiyo. Sisi, Wabunge, katika mazungumzo yetu, tunasema kwamba tuanze kubadilisha mambo yetu. Je, ni hatua gani tutachukua kurekebisha mambo haya? Kwanza, Wizara inayohusika na torati za kitaifa ambayo inasimamiwa na Waziri mhe. ole Ntimama--- Kabla yake, Waziri aliyesimamia Wizara hiyo alikuwa ni mhe. Shakombo. Itakuwaje Wizara nzima inatumia Ksh56 milion kujenga jukwaa ilhali kuna watoto maskini waliozaliwa na wapiganiaji Uhuru? Kwanza ni lazima mawazo yetu yabadilike. Siyo majengo tu yanayofaa. Tunataka watoto wale wapewe nafasi yao. Serikali iwe inahifadhi pesa. Lazima Wizara hii ya torati za kitaifa na utamaduni itenge pesa, kwa mfano, Ksh1 milioni ambazo tutapitisha hapa Bunge. Hiyo itakuwa ni bajeti ambayo tutapanga kwa ajili ya kutafuta namna ya kusaidia watoto wale wa wapiganiaji Uhuru isiwe tu kuwapa pesa za chakula. Tumetaja mambo kama vile kusimamia gharama za elimu, fedha za kuanzisha biashara na senti za kujinufaisha maisha, na kadhalika. Hilo ndilo jambo la kwanza la kufanya. Pili, inatubidi kutafuta njia ya kuwatambua jamaa hao. Watu bado wana mawazo ya kikoloni. Mtu safi aliye na mali husikizwa ilhali mtu maskini aliyevalia shuka hasikizwi. Sisi tusikomee hapa. Suala hili tumelizungumzia sana na linaelekea kutaka usaidizi wa Waziri anayehusika na masuala ya utawala wa mikoa na usalama wa ndani wa nchi lakini hayuko hapa leo. Bi. Naibu Spika wa Muda, tungesema kwamba, tunaweza kupitisha Hoja hii na isifanywe. Kitu cha muhimu ni kumwambia Bw. Mututho ya kwamba tulete sheria mpya ya Kenya ambayo tutaizungumzia kwa urefu hapa Bungeni na tuangalie kila kitu ambacho kinafaa kiangaliwe. Tunatumia njia gani na akina nani ambao watapata? Na ikiwa ni katika ile miaka, wale ambao walikuwa katika miaka hiyo iliyopita, ni kizazi gani? Tutaenda mpaka kizazi gani? Tuizungumzie na iwe ni sheria ya Jamhuri ya Kenya ambayo hakuna Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu ama Waziri anaweza kuikiuka kwa sababu tukipitisha Hoja Bungeni, mara nyingine watu wanaangalia na wanasema ni mazungumzo ya Wabunge ilhali ni kitu muhimu. Bi. Naibu Spika wa Muda, kwa hivyo, ningemalizia kwa kusema kwamba haitoshi kupitisha Hoja hii pekee yetu. Inatakakina sasa mhe. Mututho na waheshimiwa wengine ambao tunajua ukweli wa mambo na dharau ambazo zinafanyiwa maskini kwa sababu ya akili ya ukoloni, ya kwamba tupitishe sheria ambayo itakuwa haipingi mtu. Hakuna mtu ambaye atasema yeye ni mkubwa na hawezi kufuata sheria. Tutapitisha hii sheria na kupitisha pesa katika Bunge kupitia Wizara ya Toradhi za Kimataifa ili hawa watu wajulikana. Hii aibu ambayo tuko nayo itutoke. Taabu ambayo tumepata mwakani, ingine ni kutokana na sisi kutoangalia mambo ya watu ambao walimwaga damu kwa ajili ya Kenya hii. Tumewadharau watu hao na vizazi vyao na ndio October 8, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 2565 maana taabu ingine haiishi hapa Kenya. Ukabila hauishi hapa Kenya kwa sababu ni kama tumelaaniwa kwa sababu hatujafanya ukweli wa mambo. Ukiangalia nchi kama za Uingereza, Australia na Amerika, watu wametoa maombi ya msamaha. Wajeremani waliwachukua wanawake wa Kijapani na wakawafanya watumwa huko kwao lakini wanatoa pole. Na ndio nchi hizo zingine zinabarikiwa. Lakini hapa Kenya hata kusema pole kwa sababu ya kuwatesa hawa watu waliopigania Uhuru, hatujafanya. Serikali zote tatu hazifanya hivyo. Ni aibu kwetu na pia kwa nchi. Wakati umefika sasa haya yafanyike. Kwa hayo nimesema, naomba kuunga mkono."
}