GET /api/v0.1/hansard/entries/184973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 184973,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/184973/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Warugongo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 150,
"legal_name": "Nemesius Warugongo",
"slug": "nemesius-warugongo"
},
"content": "Ahsante sana, Madam Naibu Spika Wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili niunge mkono Hoja hii ambayo ni muhimu sana, na ambayo imeletwa na mhe. Mututho. Mambo mengi yamesemwa, lakini mimi pia nitasisitiza kidogo tu mambo fulani. Hao wapiganiaji Uhuru, mimi nikiwa mtoto wa mmoja wao, walijitokeza, wakamwaga damu na kuhakikisha kwamba Kenya imekuwa huru. Itakuwa vibaya sana ikiwa sisi kama watoto wao hatutakumbuka kazi yao. Watoto wa wengi waliokufa wako hai. Kuna wachache pia ambao bado wako hai. Haitakuwa vizuri kuwasahau watu hao tungoje wafe bila kuwatafutia kitu kidogo. Ningependa kupendekeza, kama vile Waziri alisema hapo awali, kwamba ikiwezekana, yale mashamba ambayo yaliibwa, kulingana na Ripoti ya Ndung'u yarudishwe, ili tuwapatie wapiganiaji wa Uhuru ambao wangali hai ama watoto wao. Tumeambiwa hapa kwamba sio Wakikuyu peke yao ambao walipigania Uhuru, bali ni kila mtu. Tumesikia maana ya Mau Mau kuwa ni \"Mzungu Arudi Ulaya, Mwafrika Apate Uhuru.\" Hiyo ni kusema kwamba sio kitu kinachohusu Wakikuyu, Wameru ama Wakalenjin. Ni kitu kinachohusu Kenya nzima. Tuko na Women Enterprise Development Fund na Youth Enterprise Development Fund ambazo zinatoa pesa kwa vijana na akina mama. Ingekuwa vizuri tuunde Freedom Fighters Fund ambayo itawasaidia wale wachache ambao wangali hai waliofanya kazi ngumu ya kupigania nchi yetu. 2568 PARLIAMENTARY DEBATES October 8, 2008 Ahsante sana, Madam Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi niongee."
}