GET /api/v0.1/hansard/entries/185622/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 185622,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/185622/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Bw, Naibu Spika, ni ukweli eneo lao lote ni Kenya. Kwa hivyo, wakiwa Nairobi wako kwenye eneo lao la uwakilishi Bungeni. Lakini sisi wengine lazima tuende, kwa mfano, Taveta tukaone wale ambao walituchagua na kutuleta hapa. Kwa hivyo, nikisema vile sikusema kwa dharau. Nilisema nikiheshimu kwamba hata wakiwa Nairobi, wako kwao. Mimi lazima niende Taveta nikaone watu wangu na niwapatia muda ili nami nizungumze juu ya maendeleo huko. Tuelewane kwenye lugha. Bw. Naibu Spika, kuna umuhimu wa sisi kurudi kwenye maeneo ya uwakilishi Bungeni ili tufanye shughulu zetu za kimaendeleo. Wabunge wapya waliochaguliwa kwenye Bunge la Kumi walisema kwamba wale Wabunge wa zamani hatujui kufanya kazi ya maendeleo. Mbona basi munang'ang'nia kukaa kwenye Bunge hili? Inafaa mrudi nyumbani ili mkafanye kazi. Msiogope wale waliowatuma kuja Bunge hili. Tufanye kazi ya Bunge kwa wakati ambao unaofaa na vile vile turudi kule nyumbani na sio kila siku kungojea hapa kuuliza Maswali na tuonekane kwenye runinga ilhali kule nyumbani hatuonekani na wala hatufanyi kazi na watu wetu. Ninaomba tuunge Hoja hii mkono ili turudi nyumbani. Kwa kawaida tumekuwa tukifanya hivyo na hatuwezi kubadilisha tabia za Bunge hili, eti kwa sababu tunaomba wiki zingine mbili. Kwani wiki mbili tunakimbilia wapi? Tuende nyumbani tukafanye kazi na turudi hapa baada ya wakati huo na tuweze kufanya kazi. Inafaa watulie. Wasiwasi ni wa nini?"
}