GET /api/v0.1/hansard/entries/185624/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 185624,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/185624/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, maswala ni mengi. Tulipochaguliwa, mwanzo mwa mwaka kulikuwa na matatizo mengi. Kulikuwa na pilkapilka za kukimbia huku na kule. Ni wakati wa kuenda kukaa na waliotuchagua na kutuleta hapa kwenye Jumba hili la kifahari na tukae na tuzungumze na wao ili tujue matatizo yao. Tutapanga vipi bajeti ya maendeleo ya maeneo Bunge kama tuko Nairobi? Tutakuwa na muda gani wa kuzungumza na watu wetu? Tunatakikana kuenda vijijini kuzungumza na wao. Na kwa wale ambao ni Wabunge wapya, nawaambia kuwa msisahau wale ambao walituleta huku. Kuna umuhimu wa sisi kuwakumbuka, kukaa na wao, kupanga mambo yetu ili tuendelee na kazi. Kwa sisi ambao ni Mawaziri, hatuogopi kazi. Tumekuwa tukiendelea na kazi, wala hatuna wasiwasi wa kazi, isipokuwa tunajua kuwa, ikiwa mmetufunga hapa na Maswali, wengine hatuna hata muda wa kukimbilia nyumbani na kuenda kutatua maswala ya kule. Kwa hivyo, tunaomba watu wote ambao walikuwa na wasiwasi wa kurudi kwa wale waliowachagua, kwa unyenyekevu warudi nyumbani ili wazungumze na wale waliowachagua. Ninafikiria bila shaka mkizungumza na wao, watakuwa na imani zaidi, na mtazidi kurudi hapa."
}