GET /api/v0.1/hansard/entries/185666/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 185666,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/185666/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Nakushukuru, Bw. Naibu Spika, kwa nafasi hii. Najiunga na wenzangu kuzungumza kwa lugha ya taifa. Naona ni dhahiri kwamba lugha ya taifa inaleta msukosuko. Maneno yanapita kando ya masikio ya watu. Tusipojaribu kuizungumza lugha hii, basi itasahaulika. Bw. Naibu Spika, nasimama kuunga Hoja hii mkono kwa nguvu zangu zote. Hiyo ni kwa sababu hii ndio mara yangu ya kwanza kuwa Bungeni. Sijawahi kupata wakati wa mapumziko na kurudi nyumbani kuwaambia watu wangu kuwa, katika muhula wangu wa kwanza wa kukaa 2462 PARLIAMENTARY DEBATES August 7, 2008 Bungeni, nimefanya hili na lile. Kwa hivyo, nawasihi ndugu zangu waliozungumza hapa kabla yangu kwamba watuonee huruma sisi tuliokuja hapa mara ya kwanza, ili tuweze kurudi nyumbani na kuwaambia watu: \"Tumetumika namna hii\". Bw. Naibu Spika, tuliapishwa tarehe 15 January, 2008. Halafu Bunge lilikwama kabla ya sisi kufanya chochote. Tukaenda nyumbani. Tuliporudi, ilikuwa mwezi wa nne. Hivi sasa, miezi saba imeisha na hatujajua mipangilio baada ya Bunge. Hatujui tunaenda nyumbani kufanya nini! Huu ndio wakati wetu wa kurudi nyumbani kupanga mipango. Wengine wetu hawajawahi kutia sahihi hundi hata moja ya CDF. Huu ndio wakati wetu wa kwenda kukaa---"
}