GET /api/v0.1/hansard/entries/185669/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 185669,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/185669/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, sisi wengine hatujatoa hata hundi moja! Tumepata pesa juzi. Hatujapanga mipango. Tunahitaji wakati huu wa miezi hii miwili angalau tuweze kurudi nyumbani na kupanga mipango. Jambo lingine, Bw. Naibu Spika, ni kwamba mambo mengi yamezungumzwa na mengi tutazungumza. Sisi tunataka kwenda kupiga siasa! Hivi sasa, kulingana na vile ile Sheria ya Bunge ya Vyama imetolewa, nataka kwenda kukifanyia chama changu kazi na kufungua maofisi ya chama katika kila sehemu ya wilaya na kuona kwamba nimetimiza yanayohitajika na sheria hiyo. Bw. Naibu Spika, ikiwa tutaendelea na shughuli zetu hapa Bungeni bila kwenda nyumbani kwa mapumziko, itakuwa kazi ngumu kwetu. Sikujua kwamba kuna kazi nyingi hapa mpaka nilipochaguliwa kuwa Mbunge. Siku ya Jumatatu, mimi na wenzangu tunafanya kazi katika vikao vya PIC. Siku ya Jumanne na Jumatano, mimi hushiriki katika vikao vya Bunge. Pia, mimi hudhuria vikao vya PIC siku ya Alhamisi asubuhi. Ninapata nafasi siku ya Ijumaa ambapo ninaenda katika eneo langu la uwakilishi Bungeni. Nikirudi hapa, nimechoka. Ninataka kuamini na kukubali kwamba mimi ni mchofu. Ninataka kumpumzika. Ninaunga mkono Hoja hii."
}