GET /api/v0.1/hansard/entries/185691/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 185691,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/185691/?format=api",
    "text_counter": 285,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bwana Naibu Spika, nimesimama hapa kidete kuipinga Hoja hii kwa kinywa kipana. Ni bayana kwamba wengi ambao wako upande wa Serikali wanaopigia debe Hoja hii ili ipite. Lakini ukichunguza kindani, utagundua kwamba wanajaribu kukwepa Maswali ambayo yamekuwa sugu hapa Bungeni. Kwa siku chache, wengi wamekuwa wakihema hapa tunapowapatia changamoto hapa Bungeni. Lakini ninataka kuwaambia kwamba mbio za sakafuni huishia ukingoni; kwani, kimo chao ki motoni kwa sasa. Bwana Naibu Spika, sisi tumetumwa hapa tuulize maswali. Maswali mengi sana hayajatimia hapa Bungeni. Hatujapewa majibu ya kutosha. Mimi mwenyewe ninatarajia kujibiwa Maswali manne. Bwana Spika aliniambia kwamba kwa siku kumi yatafika Bungeni. Lakini Bunge likihairishwa inamaanisha changu kitakuwa kimezama kwenye bahari ya sahau. Nikasema ni lazima nipinge Hoja hii. Vile vile, tuna miswada kadhaa. Tulikuwa tunataka kubadilisha Katiba ama sheria fulani ili tushugulikie wale wazee wa mitaa. Tunataka kupitisha Mswada hapa Bungeni walipwe mishahara. Wanangoja kwa udi na uvumba waone kwamba marekebisho haya yametimia. Hatutaenda nyumbani kwa sababu ya jambo hilo. Bw. Naibu Spika, pili ni kwamba, sisi kila wakati tumekuwa tukishika kiguu na njia kuelekea nyumbani. Kila Jumaa wengine wetu tunatoka hapa kwenda kushughulikia maswala ya wananchi. Lakini kuna wale wachache ambao wanaponda raha hapa Nairobi. Tunataka kuwaambia August 7, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 2467 kwamba wakati sio huu. Sisi tunataka nafasi ya kutosha tuketi hapa Bungeni. Wengine wamesema kwamba, kuna zile hundi ambazo zinatakikana kupeanwa. Tayari mimi mwenyewe, kupitia pesa za dharura, mimeweza kupeana hundi kama tano ambazo ni jumla ya Kshs1 milioni. Wale Wabunge wengine watajaribu kueleza wananchi wao wamekuwa wapi wakati huo wote ikiwa wengine kama mimi tumepeana hundi zaidi ya Kshs1 milioni."
}