GET /api/v0.1/hansard/entries/185693/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 185693,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/185693/?format=api",
    "text_counter": 287,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bwana Naibu Spika, sisi tuna maswala hapa. Mheshimiwa fulani hapa ameeleza kwamba kumekuwa na kutoelewana kati ya Wabunge na Mawaziri kwa maswala ya madiwani. Hatutaenda kuulizia kule nyumbani maswala ya madiwani kwa sababu itakuwa ni poroja na propaganda . Tutaulizia hapa Bungeni kama tunataka majibu ya kutosha. Vile vile, sisi tumekuwepo hapa, juzi mwezi wa sita, baada ya kutoka likizo. Ukifanya hesabu utagundua kwamba tumekuwa Bungeni miezi miwili. Nafikiri ni kufedhehesha pakubwa sana na sisi wenyewe hatutakuwa tunafanya jukumu letu la kuwatimizia Wakenya malengo ambayo walituleta Bungeni. Tutakuwa tunafuja pesa za wananchi ikiwa kila wakati tutakuwa tunakaa nje ya Bunge kutoshugulikia maswala yao. Ninasimama hapa kusema kwamba tunahitaji wakati kabambe wa kushughulikia maswala yanayowasumbua Wakenya. Mimi mwenyewe ninasikitika kwamba, kwangu kuna uvamizi wa usiku na mchana. Mahala ambapo nitatafutia majibu ya kutosha, mwelekeo na muundo msingi wa kuweza kuweka mambo ya usalama kule kwangu, ni hapa Bungeni. Inafaa Waziri wa Usalama atupatie muelekeo sawa sawa. Hatutaenda kuulizia kule nje, kwa sababu tutakuwa vyura vya kupiga kelele huku ng'ombe wakiendelea kunywa maji. Kwa hivyo, ninataka hapa Bungeni tukumbatiane na wale ambao wako upande wa Serikali kulingana na maswala ambayo yamo katika taifa la Kenya. Bwana Naibu Spika, nikikunja jamvi, ninataka kusema kwamba tuna ripoti ya Hoteli ya kifahari ya Grand Regency. Lazima tupate ukweli wa kutosha. Ninashukuru kwa nafasi ambayo umenitunuku. Ninakuheshimu kwa heshima zangu zote na ninakuvulia kofia. Ahsante sana."
}