GET /api/v0.1/hansard/entries/185731/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 185731,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/185731/?format=api",
"text_counter": 325,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Haji",
"speaker_title": "The Minister of State for Defence",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, nakushukuru. Nataka kuchukua nafasi ili niunge mkono mjadala ambao unaendelea. Kama tunavyojua kama Wabunge, punde tu tulipochaguliwa na wananchi hatukupata nafasi ya kuweza kuketi na kutafakari na kushauriana na wao juu ya mambo yale ambao wangetaka sisi kuweza kutekeleza kama wajumbe wao, kwa sababu wakati huo mvurugano na shida kubwa ilitokea katika nchi yetu. Hilo lilikuwa August 7, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 2475 jambo ambalo lilitutia sisi wote wasi wasi kwa sababu hatukujua mwelekeo wa Kenya wa kesho utakuwa namna gani. Bw. Naibu Spika, tunavyojua kama taifa, tulikuwa tunapokea majirani wetu ambao nchi zao zilikuwa na vurugu na wamepata hifadhi hapa. Kwa hivyo, wengi wetu tulikuwa na wasi wasi kwamba nchi yetu ikiharibika tutaenda wapi. Sasa tumepata nafasi ya kuweza kukaa pamoja katika Jumba hili ili tujuane na tumeweza kufanya kazi ile ambayo tumefanya mpaka siku ya leo. Nafikiri wakati umefika wa sisi kupata nafasi ya kuweza kurudi nyumbani kwa muda mrefu kulika mwisho wa wiki pekee yake kukaa na wananchi. Hasa, nataka ndugu zangu wajue kwamba sisi ambao tunatoka mkoa wa Kaskazini Mashariki, tunasafiri kwa siku mbili ndipo tufike katika maeneo yetu ya uwakilishi Bungeni na wakati mwingine kukinyesha hata inaweza kutuchukua wiki nzima kufika. Mimi najue katika eneo langu la Ijara, kwa miezi minne hakuna hata gari hata ikiwa Land Rover ambayo inaweza kupita kwa sababu ni ardhi ya mchanga mweusi. Hii likizo itatupa fursa ya kuenda kukaa na watu wetu na kushauriana nao. Na sio hio pekee yao. Tunasikia Wabunge wanafanya sherehe ya kupongeza watu wetu kwa kutuchagua. Hakuna sherehe muhimu kama Mbunge kuenda kukaa na watu wake kwa wiki tatu na kunywa chai na wao, hata chini ya miti na kubadilishana maoni. Isitoshe, Bw. Naibu Spika, hii itatusaidia pia kuzungumza na watu wetu na kuleta maridhiano ili, wale ambao wanagombana waweze kuletwa pamoja chini ya uongozi wa Mjumbe ambaye amechaguliwa. Bw. Naibu Spika, sio vizuri kwa sisi kupuuza yale mambo yanatokea katika mashule. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kenya, zaidi ya shule 270 zimegoma. Siyo kugoma peke yake! Wanafunzi wamearibu vifaa vingi na majengo! Mambo hayo yote hayawezi kusuluhishwa bila ya viongozi kukaa na wananchi na kujua ni nini hasa kinawafanya vijana wetu kufanya yale ambayo wanafanya. Pia, zile kamati ambazo zimeundwa kwenda kuingilia mambo kama hayo, zitapata nafasi zaidi kuliko wakati Bunge linapoendelea, kuweza kutembelea kila sehemu na kujua yale mambo yanayoendelea. Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, hata katika fikira zetu sisi wenyewe, tukikaa katika Jumba hili--- Juzi, Bw. Spika alisema kwamba kuna mtu ambaye amehisi joto. Ni kweli! Alihisi joto kwa sababu kila mara tunapiga kelele, tunazungumza na kubishana; hata vichwa vinauma! Kwa haya machache, Bw. Naibu Spika, naunga mkono."
}