HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 187323,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/187323/?format=api",
"text_counter": 289,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Machage",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Roads",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": " Naibu Spika wa Muda, shukran kwa kunipa wasaa huu kuunga Hoja hii mkono. Ingawa nimechelewa, ninafikiria ni Hoja ya maana na 2210 PARLIAMENTARY DEBATES July 30, 2008 lazima izingatiwe kusudi tuwe na msingi kamili wa kuiongoza nchi hii. Wazee wa nyumba kumi kumi huko vijijini wana kazi ya kuwasaidia machifu ama naibu wa machifu kwa daraja hilo. Kama vile wanavyoitwa, kazi zao zimepanuka na wakati huu sio nyumba kumi kumi tena. Wanaangaza kazi zao kwa nyumba zaidi ya 100 hata 1,000 kwa wakati mwingine, bila malipo. Naibu Spika wa Muda, nafikiria ni kunyanyaswa kwa hali ya juu kwa kutowalipa marupurupu yao. Wengi wao wamejitolea na wanaheshimu sheria. Lakini kitengo cha saba cha sheria kinachoangaza kazi za chifu, lazima tukigeuze. Hatuna budi, kama Bunge hili linalounda sheria, kukigeuza hiki kitengo kusudi hao wazee wapate malipo yao. Ninaamini kwamba wakishapata marupurupu yao, watafanya kazi zao ambazo ni za ziada vizuri zaidi. Wakati mwingi mambo ya usalama hupoteza lengo lake wakati habari muhimu hazikusanywi mashinani. Ni kama vile kujenga nyumba bila msingi. Hawa wazee, wakiwa wanaume na wanawake ndio msingi wa usalama na habari za ziada ambazo zahitajika kabisa katika kuangaza hasa uongozi wa utawala mikoani. Hao wana uwezo wa kujua ni nani amefika kwa kijiji, nani mhalifu, nani mgeni, nani ameiba kitu fulani na amekileta kijijini, kama vile ng'ombe, ni nani hakulala kijijini na kadhalika. Haya ni muhimu, kwa sababu, wakati mwingine ni lazima habari kama hizi zikusanywe ili kuangaza hali ya usalama wa nchi. Naibu Spika wa Muda, iwapo Serikali kuu inataka huduma za hawa watu lakini haitaki kuwapa mishahara yao, ninafikiri wao wenyewe wanavunja sheria ya kiutu na ubinadamu. Lazima hao pia waangaliwe kama watu ambao wamejitolea kuitumikia Serikali hii na wapewe kilicho chao. Ya Kaisari ipewe Kaisari. Kuna mambo mengi ambayo hawa watu wana faida kwetu. Katika mambo ya elimu, hawa wazee hujuwa kwamba mzazi fulani anakebehi sheria ya kupeleka watoto shuleni, amekataa au hana uwezo. Hawa ndio wataleta ripoti kamili, kwamba mji huu hauna uwezo wa kupeleka mtoto shuleni au mji huu umekataa kata kata kwamba watoto wao wasome. Hizo habari zitatumika vizuri, hasa, kwa minajili ya kuhakikisha kwamba kila mwananchi wa Kenya amesoma na kuhitimu hadi kiwango cha darasa la nane kwa wakati huu na hapo baadaye labda kidato cha nne. Bi. Naibu Spika wa Muda, kuhusu afya, wazee hawa watatoa ripoti mara moja iwapo kutazuka ugonjwa ambao utahitaji huduma za dharura. Wazee hawa wana uwezo wa kutoa ripoti kamili kuhusu idadi ya watu waliopata ugonjwa katika kijiji. Watatambua ni watu wangapi wamepuuza kwenda kutibiwa na ni watoto wangapi hawajawahi kupata chanjo. Hii ni habari muhimu sana kwa sababu inasaidia kufanya hesabu ya gharama hasa kwa huduma za chanjo. Hata kuhusu kilimo, wazee hawa watajua ni nani amepuuza kwenda shambani msimu fulani. Wanawajua wale ambao kazi yao ni kuitisha tu msaada wa chakula cha bure ilhali wana mashamba yanayoweza kulimwa. Wazee hawa watajua ikiwa kuna njaa na chakula kimeletwa, ni familia gani zilizoathirika zaidi. Wao ndio watasema, \"Bwana Chifu, wacha kumdhulumu fulani kwa sababu hakufanya makosa.\" Wazee hawa wana faida kubwa. Wao wanaweza kupindua mawazo ya wananchi hasa wakati wa kutangaza sera za nchi hii. Wakati huu tuko katika harakati za kujaribu kuangaza mambo ya kugeuza Katiba hii ili iwe kamilifu katika kuhudumia wananchi wa Kenya. Wazee hawa watatumika kuwaongoza, kuwaambia na kuwafundisha wale wananchi vijijini faida na hasara za kubadilisha vitengo fulani katika Katiba. Wana huduma kuu ambayo inahitajika kabisa hasa katika uongozi wa nchi hii. Sisi tunawaita wazee wa nyumba kumi kumi. Ni muhimu wawe hivyo ili waangaze miji kumi ndipo waweze kujua kinachotendeka mashinani. Iwapo ni wachache katika tarafa fulani, basi waongezwe ili wawe wengi zaidi. Sheria ya kutambua kwamba wazee hawa si vibaraka wa chifu iwekwe. Lazima pawe na sheria ya kusema kwamba kabla ya kuteuliwa kuwa mzee wa nyumba kumi kumi, sharti uwe mzee mwenye tabia na kisomo fulani. Sio kisomo cha darasani tu! Kwenda darasani haimanishi July 30, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 2211 umesoma! Huenda ukawa na shahada ya digri lakini iwe huna hekima. Kwa hivyo, kuna kisomo cha aina nyingi. Huyu ni mzee ameona mengi. Yeye huenda kwa mabaraza ya chifu kila wakati. Vile vile yeye huenda kwenye warsha nyingi. Kwa hivyo, amepanua mawazo yake. Ni mzee anayeelewa mambo. Hana kichaa na si mwizi. Ni mzee asiye na madharau. Ni mtu wa watu. Lazima kuwe na sheria ambayo itaangaza kwamba yule atakayeteuliwa kuchukua madaraka hayo ni mtu wa aina gani. Je, ni kiongozi ama ni mtu wa kunyanyasa binadamu? Hoja hii iliyoletwa na mhe. Wamalwa imekuja wakati mzuri. Hatuna budi sisi Wabunge kuangaza mawazo yetu kwa jambo hili la dharura na kuliweka maanani. Ni jambo muhimu na kwa hivyo tulipitishe bila kupinga. Asante, Bi. Naibu Spika wa Muda."
}