GET /api/v0.1/hansard/entries/187327/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 187327,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/187327/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kutuny",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "Nashukuru sana, Bi Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii ya kurekebisha Sheria ya Chifu ili kubuni ofisi ya kiranja wa mtaa, ama wazee wa mtaa na kuweko kwa sheria kabambe ya kuidhinisha malipo yao. Wao huchangia pakubwa ufanisi wa mashinani. Kule kwetu, wao hutambulika kama wazee wa mtaa, na wamechangia pakubwa sana utatuzi wa matatizo yanayokithiri mashinani. Kukiwepo na kutoelewana baina ya jamii na pia kutofautina kwa familia, wao ndio huingilia kati kutatua shida hizo. Pia wanashirikiana bega kwa bega, mithili ya mchwa na nyuki, na wazee ambao wana taathiriba ya muda mrefu katika matatizo yanayokumba jamii. Kwa sasa matatizo mengi yanawakumba wazee wa mtaa, na wanajiingiza katika kutafuta mlungula, au kiinua mgongo, kwa sababu hawajikimu kimaisha. Watu ambao wana pesa katika jamii, wanawatumia kutotatua matizo jinsi wanavyotaka. Sheria hii ikiletwa Bungeni na ipitishwe, hali ya kiinua mgongo kule mashinani itafutiliwa mbali. Kila mwananchi atakuwa na nafasi nzuri ya kuwasilisha kesi na kusikizwa kwa njia mwafaka. Pili, wazee wa mtaa ndio macho ya Serikali siku hizi. Kule kwetu kumekidhiri wizi wa mifugo na wao ndio wamekuwa wakitupasha sisi na Serikali habari jinsi wizi unavyoendelea. Hii ni kumaanisha kwamba ikiwa Serikali itawapa nguvu, matatizo yale yanaweza kutatuliwa kwa namna rahisi. Vile vile kumekuwako na ruwasa, ama ajenda, tofauti tofauti ya Serikali. Katika mipango ya Serikali imeonekana kwamba kuna mpangilio fulani wa taarifa za Serikali - kutoka juu hadi chini - kufika mashinani; lakini zikifika kwa naibu wa chifu zinakwama pale. Wazee wa mtaa hawana hari, ama motisha, ya kuwapasha wananchi habari kwa sababu wana upungufu, labda wa nauli ya kusafiria kutoka kituo kimoja hadi kingine. Bi Naibu Spika wa Muda, watu hao wakipewa hela kidogo kama mshahara, kunaweza kuchangia pakubwa kwao kuwapasha wananchi taarifa tofauti tofauti za Serikali. Nikizungumzia malipo, ningependa kusema kwamba katika taifa la Kenya, kuna mabepari ambao Serikali inawalipa kitita cha zaidi ya Kshs2 milioni kwa mwezi. Tunasema tunataka Serikali ichukue hatua. Ndiyo maana tunaiunga mkono Hoja hii. Kama Justice Ringera analipwa Kshs2 milioni kwa mwezi, tatizo liko wapi Serikali ikipungunguza hela hizo na kumpa mtu mwingine ambaye anashughulikia matatizo ya Wakenya wengi? Serikali inaweza kuwalipa watu hao Kshs1,000 kila wiki ili waweze kupata Kshs4,000 kwa 2214 PARLIAMENTARY DEBATES July 30, 2008 mwezi. Hatua kama hiyo itawawezesha Wakenya kupata huduma kwa njia moja ama nyingini kwa urahisi. Mengi yamesemwa juu ya Hoja hii. Ninaamini kwamba hatutakuwa na budi yoyote ila kuipitisha halafu iwe sheria ili Wakenya waweze kupata huduma kwa njia mwafaka na rahisi. Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii, ninapochukua kiguu na njia kwenda kutafuta maankuli ya mchana. Asante sana."
}