GET /api/v0.1/hansard/entries/18878/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 18878,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/18878/?format=api",
"text_counter": 555,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, utakuta kuwa hivi juzi nchi yetu ilishambuliwa na maharamia wa baharini. Tungekuwa tuna vifaa vya anga za juu, tungeweza kuwatambua mapema na kutumia vikosi vyetu vya ardhini na majini kujua ni wapi hasa hawa maharamia walipokuwa; lakini kwa sababu Serikali haijachukua majukumu ya kuhakikisha kuwa ujuzi na utaalamu wa sayansi na teknolojia ya angani zimesitawishwa vizuri mpaka wakati huu bado ujuzi uko mikononi mwa wageni. Baada ya miaka 40 ya Uhuru, naona kuwa Serikali yetu, wakati umefika iamke na iangalie itafanya nini."
}