GET /api/v0.1/hansard/entries/18879/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 18879,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/18879/?format=api",
    "text_counter": 556,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ni jambo la kushangaza kusikia Waziri akisema kuwa kitengo hiki kiko mikononi mwake na hakijaanza kufanya kazi. Je, kama hakijaanza kufanya kazi, wao wanatarajia nani wahakikishe kuwa kinaanza kufanya kazi? Ukiangalia kama eneo Bunge lile ninalotoka lina wanyama wengi na Mhe Otichilo, katika kazi yake ile alikuwa anafanya, alikuwa anashugulika na mambo ya wanyama, ndovu, chui, simba na kadhalika. Mara nyingi wanyama hawa huingia katika mashamba ya watu na kuharibu mimea. Kitambo ndege itumwe kutoka Nairobi ifike Taita, mimea itakuwa imeharibiwa, watu wamekufa na kadhalika. Tungekuwa na hivi vifaa, vingeweza kuangazia na tukajua hawa wanyama wako wapi na kutuma askari ambao hulinda wanyama kuhakikisha kuwa madhara ambayo yangetokea yamezuiwa au kupunguzwa."
}