GET /api/v0.1/hansard/entries/190312/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 190312,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/190312/?format=api",
"text_counter": 28,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms. Leshomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Bw. Spika, naomba kumuuliza Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani Swali Maalum lifuatalo. (a) Je, Waziri ana habari kwamba kuna vita vikali baina ya jamii za Turkana na Samburu vinavyoendelea katika tarafa ya Baragoi na Ng'iro katika eneo la Samburu Kaskazini, ambapo wahalifu kutoka jamii ya Turkana wameshambulia manyatta za watu wa jamii ya Samburu, wakaiba takriban ng'ombe 400 na kuua watu kadhaa? (b) Waziri ana habari kwamba watu kutoka jamii ya wa Pokot vilevile wanaendelea kuwashambulia jamii ya wa Samburu katika tarafa za Kirisia na Loroki katika eneo Bunge la Samburu ya Kati? (c) Serikali imechukua hatua gani kuhakikisha kwamba mifugo walioibwa, ambao wako malishoni karibu kilomita 25 kutoka eneo la mashambulizi, wamekombolewa na kurejeshewa wenyewe? (d) Serikali ina mipango gani hasa kukomboa mifugo wote walioibwa na kuhakikisha visa July 8, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 1663 vya mashambulizi na wizi wa mifugo vimekomeshwa kabisa katika maeneo hayo?"
}