GET /api/v0.1/hansard/entries/19278/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 19278,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/19278/?format=api",
    "text_counter": 354,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii. Hoja hii imezua maswala mengi ambayo yanaweza kuleta majonzi kwa wananchi wetu. Ninakumbuka nilisimama hapa na kupinga uteuzi wa Bw. Kosgei kama mkurugenzi wa shirika hili. Hii ni kwa sababu katika mahojiano, yeye alikuwa wa nne. Bw. Abdi ndiye alikuwa wa kwanza na kufuatiwa na Bi. Eva Owuor. Kulikuwa na mwingine aliyekuwa wa tatu. Je, ni kwa nini Abdi hakuteuliwa kama mkurugenzi wa shirika hili? Je, alikataa kuteuliwa kwa sababu ya kabila lake au hakuwa na uhusiano wowote na wakubwa wa Wizara hii? Je, huyu Bw. Kosgei ni ndugu wa Waziri Msaidizi katika Wizara hii au alikuwa na uhusiano wa karibu sana na Katibu Mkuu? Haya tu ni baadhi ya maswali ambayo hata sasa yanahitaji majibu. Ninakumbuka vizuri pia bodi ilipinga uteuzi huu, lakini Waziri akamteua Bw. Kosgei. Iwapo mambo yataendelea namna hii, basi taifa letu litaangamia. Taifa letu limekuwa kama mtu ambaye alifungua kampuni yake ya kibinafsi na kuajiri mkurugenzi. Lakini kwa vile hakumwamini mkurugenzi huyu, akaajiri naibu wake na askari 15 wa kumlinda. Mwishowe, pesa zilitumika kulipa mishahara ya watu hawa na kampuni yake haikupata faida yoyote. Pesa ambazo alitumia kuwalipa askari zilikuwa ni zaidi ya zile ambazo alimlipa mkurugenzi na msaidizi wake ili awalinde wasiibe. Leo ukisimama unajiuliza; je, chanzo cha mambo haya ni nini? Tumepata Uhuru wetu karibu miaka 50 iliyopita. Katika uongozi wa hayati Jomo Kenyatta na Jaramogi Oginga Odinga akiwa Makamu wa Rais, nchi ilikuwa na mgawanyiko na kisingizio cha mgawanyiko kilikuwa ni kwamba, Kenyatta, Jaramogi, Ngei na wale wengine waliongoza idadi kubwa ya wakenya ambao hawakuwa wamesoma na hawakuelewa undugu wa Mjaluo na Mkamba ni nini. Tulivumilia mambo hayo yote na tukastahimili tukiomba Mungu kwamba, miaka 20 itakayokuja, kizazi ambacho hakikuwa kikielewa umoja wa Wakenya kitakuwa kimepita na kizazi kipya kimekuja. Ukiangalia leo na wakati wa hayati Kenyatta na wenzake, ni dahiri na wazi kwamba, kasheshe tuliyo nayo ya kikabila katika taifa letu imepita ilivyokuwa wakati tuliponyakua Uhuru. Je, taifa hili linaelekea wapi? Hapa tunazungumza kama Wajumbe lakini mtu akiteuliwa kuwa Waziri, ukiingia afisi yake, utapata kuwa karani, msaidizi na askari wake wote wametoka kabila lake, halafu anasimama hapa kuzungumza maswala ya umoja wa taifa la Kenya. Umbwa mwitu tunavaa mavazi ya binadamu, lakini rohoni sisi tunataka kutafuna na kukanyaga wanaostahili kusaidiwa. Mimi nilipochukua afisi ya Whip, nilipata msichana mmoja Mluhyia na Wakikuyu wawili. Hadi sasa, sijaleta Mkamba pale. Katika afisi yangu ya kazi, ninadhirisha hapa kwamba karani wangu ni Mluhyia, mhandisi mkuu wa kuchimbua madini ni Mjaluo na mkuu wa hesabu ni Mkikuyu. Ninaweza kuzungumzia utaifa. Ukienda kila ofisi kutoka kwa ofisi ya Rais kuteremka, ofisi ya Waziri Mkuu, ofisi ya Makamu wa Rais, utaona ukabila ulioko. Halafu tunakuja hapa kujifanya kwamba tunaongoza kwa haki. Katika Bunge hili, kuna Mswada wa kamati ya Bunge, the Parliamentary Service Commission, ambao unasema kwamba, walioko ndani wameajiri watu wao. Wameleta watu wao pale. Mimi sijathibitisha haya, lakini kama Kiranja wa Serikali, ninataka kuthibitisha kama ni kweli ndio nijue nitatetea mambo hayo namna gani. Lakini ikiwa ni namna hiyo, taifa hili limeangamia. Sisi wasomi, wenye ujuzi na wenye kupewa madaraka ya kuongoza, kitu cha kwanza ambacho tunazungumza kama mawaziri ni kupeleka bendera Ukambani na kwenda kuwaambia Wakamba kuwa: “Mnaona mmenichagua na chama fulani, basi, nimepata bendera na hii bendera ni yenu ya kura”. Ni kiongozi mgani ambaye anaitisha kura kuongoza Wakenya ijapokuwa kuitisha kura watu wake wafike Ikulu ili wale? Tukifundisha watu namna hiyo, kashehe inaanza. Hakuna anayeingia Bunge hili ambaye ana usalama nyumbani, kwa sababu, Wakenya wameamini kwamba uwe umefaulu namna gani, uko na ujuzi namna gani na uwe mwaminifu namna gani, kama haujapanda kwenye mabega ya ndugu yako au dada yako, hauwezi kuona usawa wa taifa hili. Hii ndio kazi katika taifa letu leo; hata wafanyakazi wa Bunge hili. Ofisa akitaka madaraka anaangalia Mhe Muthama ana uwezo gani, ama Mhe Muthama ndiye nani. Anatakia azungumze ili apate madaraka. Hii ni kwa sababu hata ukifanya kazi kama punda katika taifa hili, huwezi kupandishwa cheo mapaka ndugu, mama au nyanya yako awe katika ofisi hiyo na azungumze kwa niaba yako ndipo upate madaraka. Kila kitu katika Kenya kinahusu rushwa na kuzungumzia. Halafu unapomshika mtu mkono na kumpeleka kazini, hiyo kazi hafanyi kwa sababu ana Mungu wake aliyempeleka katika hiyo nafasi. Akishindwa na kazi yake, kitu cha kwanza atafanya ni kukimbia kwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Rais mwenyewe au kaka yake na kumwambia: “Kwa sababu mimi ni kabila hili naonewa; hii ni kwa sababu mkubwa ofisini ni kutoka kabila hi”. Hii ndiyo sababu kazi ya taifa haiendelei."
}