GET /api/v0.1/hansard/entries/19282/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 19282,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/19282/?format=api",
"text_counter": 358,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Leo tuna simu na unaiweka mfukoni na unaweza kuongea hata ukiwa kwa ndege. Nakuambia leo kati ya koo pale Laisamis watu 40,000 hawajahi kupiga simu hata siku moja. Hakuna nework! Kutoka pale mpaka Isiolo, hao watu pahali wananunua nyanya na kitunguu ya kupikia chakula, ni kilomita 170. Hiyo ndio soko. Wezi hapa wanachukua Kshs15 milioni na kuigawa ikiwa juu ya meza kwa madai kuwa wanatafuta mkurugenzi mmoja wa kampuni, na hali watu kama wale wa Laisamis hawana maji au hospitali. Nakuambia kitu kinachoitwa dispensary hamna katika hiyo sehemu. Mhe Lekuton anawakilisha sehemu ambayo ukubwa wake ni kilomita 24,000 mraba. Akitoka hapa kwenda mwisho wa sehemu hiyo ya uwakilishi Bungeni, anaweka magurudumu mapya ya gari na akifika kule mwisho anayabadilisha. Asipobadilisha akifika mwisho wa sehemu hiyo ya uwakilishi Bungeni, hawezi kurudi alikotoka. Je, hii ni Kenya ambayo iko na watu wenye matumbo kama gunia? Wanakula Kshs15 milioni ili kuajiri mtu mmoja? Mwishowe wanawaandikia Wakenya mtu ambaye hajafaulu kuingia katika ile nafasi. Taifa hili lina uchungu. Maisha ya Wakenya ni ya uchungu. Mambo haya yakome kabisa. Ni dhahiri kwamba Rais mwenyewe, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, katika ofisi wanazokalia, tunataka kuona uwezo wa uongozi unaonekana. Hakuna mahali tunaenda kama mtu mmoja anaweza kusababisha mambo haya na anakula na kulala na kupeleka watoto wake kwa masomo ya juu, ilhali katika sehemu kama ile nimetoka, watoto kwenda shule ni bahati. Kutoka shule moja hadi nyingine ni kilomita 15. Kule sikuona matatu na macho yangu. Gari kule ni punda. Je, hao sio Wakenya? Je, pesa hizo haziwezi kutumiwa kwa hao watu? Kwa nini katika taifa letu la Kenya Mbunge anapochaguliwa na kuwa Waziri, baada ya miaka mitano, anaanza kujenga nyumba na kununua ndege ilhali alikuwa na kijigari kimoja kwa miaka mitano? Je, pesa hizo zinatoka wapi?"
}