GET /api/v0.1/hansard/entries/19283/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 19283,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/19283/?format=api",
    "text_counter": 359,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kumalizia nikiwa na machungu sana katika moyo wangu. Ningependa kusema kwamba Kamati hii imeweza kutoa mwelekeo ambao ukifuatwa, utakuwa ni funzo kwa wale wanaofanya mambo kama haya. Ile Bodi yenyewe inafaa kuthibitisha ilitumia Kshs15 milioni kununua nini na walikuwa wanaajiri watu wangapi. Kazi yao ilikuwa ni nini ili watumie Kshs15 milioni. Kama ni mwanzo wa mambo, wahusika wanafaa kurudisha pesa hizo ndipo mambo haya yakome. Itakuwa ni vigumu sana mimi mwenyewe kupanga kuiba. Kama Whip katika ofisi hii, nikienda kwa ofisi za makarani na kuwaambia kwamba nataka waniwekee hizi pesa, nikitoka haiwezekani kwamba yule karani atakataa kuiba. Mimi mwenyewe lazima nikae kwa ofisi na kukataa wizi ndio katibu wangu asiibe kwa sababu ananiogopa na kuniheshimu. Lakini ikiwa mimi ndio kinara wa kuweka msingi wa mambo hayo, ni jambo la kuudhi. Ni kama yale mambo tunayoendelea nayo sasa ya shule. Sisi tulikaa kama Kamati ya Bajeti na kutafuta pesa ya kuajiri walimu. Lakini kufika hapa, inakuwa ni kazaazaa kama ule mpira uliochezwa na Kenya na Uganda. Ilikuwa pata shika; iko, hakuna. Mara inalipa kodi, mara inafanya hii. Sisi tulitafuta pesa na wenzangu mmoja wao yuko hapa, mhe. Koech. Pesa zilikuwa bila utata wala kuhusisha mambo mengine au kuleta kasheshe. Nafurahi kuwa mwishowe, pesa za walimu ziliweza kupatikana. Ni lazima tusimame kidete na kutetea mambo haya ili tuendelee mbele."
}