GET /api/v0.1/hansard/entries/192941/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 192941,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/192941/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kambi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 39,
"legal_name": "Samuel Kazungu Kambi",
"slug": "samuel-kambi"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Mimi ni mmoja wa waheshimiwa Wabunge wanaoiunga mkono Hotuba ya Waziri wa Fedha. Hotuba hii ilijikita katika sera tatu: Sera ya uchumi, mfumo wa jamii na itikadi za kisiasa. Hakuna nchi yoyote inayoweza kuendelea ikiwa haina barabara nzuri. Ninamshukuru Waziri wa Fedha aliikumbuka bandari yetu ya Mombasa na kuitengea kiasi fulani cha pesa zitakazotumika kuitayarisha kuwa bandari huru. Tunamshukuru sana Waziri kwa jambo hilo. Bw. Spika, nchi yo yote ile haiwezi kusema imeendelea kama haina chakula cha kutosha. Ukiiangalia Bajeti, utaona kwamba Waziri wa Fedha ameipa Wizara ya Mipango Maalum kiasi kidogo cha pesa licha ya kwamba nchi hii inakumbwa na baa la njaa. Je, pesa zilizotengewa Wizara hii zitatosha kweli? Vile vile, nchi yo yote ile, haitaweza kusema kwamba ina maendeleo kama haina wawekezaji. Tunamshukuru Waziri kwa kurahisisha uwekezeji humu nchini kwa kupunguza idadi ya leseni zinazohitajika. Kuhusu usimamizi bora wa Benki, Waziri ameongeza kiasi cha chini cha pesa zinazohitajika kuanzisha benki, kutoka Kshs250 milioni hadi Kshs1 bilioni. Hatua hii itawafanya watu wenye pesa chache kuumia. Kwa hivyo, ningependa kuliomba Bunge hili kuhakikisha kwamba kile kiwango cha zamani kimedumishwa. Bw. Spika, huhusu sekta ya maji, kama wanavyosema wahenga, binadamu ni maji. Pesa zilizotengewa Wizara ya Maji na Unyunyizaji Mashamba hazitoshi kupeleka maji kila mahali nchini. Ninashukuru kwamba mapato yetu kutokana na ukusanyaji wa ushuru yameongezeka. Lakini, sikubaliani na Waziri katika pendekezo lake la kuyatoza ushuru marupurupu ya Wabunge. Hivyo ni kusema kwamba Wabunge wazidi kuwa maskini. Mishara yetu tayari inatozwa ushuru. Marupurupu yetu yakitozwa ushuru, tutakuwa maskini zaidi katika nchi hii. Bw. Spika, katika Hotuba yake, Waziri aliongea kuhusu uchumi wa jamii. Kuna vijana ambao hawana kazi. Pesa zilizotengewa Hazina ya Biashara ya Vijana hazitoshi. Tunaomba pesa hizo ziongezwe, kwa sababu vijana hawana kazi katika nchi hii. Kama unavyojua, vijana hawapewi nafasi ya kuhudumu Serikalini kwa sababu wazee bado wanahudumu Serikalini kama Makatibu wa Kudumu. June 19, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 1283 Kwa hayo machache, ninaiunga mkono Hoja hii."
}