GET /api/v0.1/hansard/entries/193116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 193116,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/193116/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii kutoa maoni yangu kuhusu Bajeti ya 2008/2009. Mimi niliguswa sana kuona kwamba tunahitaji pesa nyingi za kuagiza chakula kutoka nchi za nje ili kuwalisha Wakenya kwa miezi michache tu. Huku nikimshukuru Waziri wa Fedha kwa makadirio ya pesa ambayo yanafaa sana, vile vile nasikitika kwamba nchi inahitaji mipango kabambe kuliko kuletewa chakula kutoka nje. Nasema hivyo kwa sababu mabilioni ya pesa tutakazotumia kuwanunulia wananchi wa Kenya mahindi yangefaa kutumiwa kuwapatia maji. Tungewaacha wahangaike kwa hiyo miezi mitatu! Nchi ya Kenya ni kubwa. Sehemu kubwa ya kule ninakotoka ina rutuba nyingi sana. Kile wananchi wanachokosa tu ni maji. Tukiwapatia maji, hawatahitaji kupewa chakula. Bw. Naibu Spika wa Muda, utakubaliana nami kwamba taifa ambalo haliwezi kulisha watu wake ni taifa maskini. Liwe ni taifa lililo na barabara nzuri au hospitali nzuri, lakini likiwa haliwezi kuwalisha wananchi wake basi taifa hilo ni maskini. Tunalalamikia bei ya vyakula. Inaonekana kwamba kuna watu fulani ambao wana njama ya kuleta chakula humu nchini ili wafanye biashara. Tunapozungumzia masuala kama vile kupunguza ushuru unaotozwa chakula kinacholetwa humu nchini, hilo halisaidii kwa vyovyote kwa sababu wafanyabiashara ambao wamewanyonya wananchi kwa miaka hii yote ni wanafiki na wanangojea tena wakati ufike ili waendelee kuwanyonya wananchi. Kwa hivyo, hakuna njia yoyote ambayo bei ya chakula itaweza kuteremka. Mapato ya wananchi wa Kenya ni takriban asilimia 85. Hii ni hali duni sana. Soko ni moja ambalo wananchi na Wabunge wananunua bidhaa. Mishahara ya wananchi huanzia Ksh3,000 na ikiwa zaidi ni Ksh10,000. Wanalipa nauli ya usafiri. Bei ya sukari na majani chai ni ile ile. Itakuwaje wanaomiliki hizi biashara wateremshe bei ya bidhaa hizi ili kuwasaidia wananchi? Mimi natoa mwito kwa Serikali na hasa Waziri wa Fedha, akadirie fedha zaidi kwa sekta ya maji ili wananchi wa Kenya waweze kujilisha. Bw. Naibu Spika wa Muda, juzi askari jela waligoma. Polisi wanafanya kazi katika hali duni sana. Nyumba wanamoishi si nyumba utatarajia mtu anayetoa ulinzi kwa taifa kuishi ndani. Sote tumeona jinsi wanavyoishi. Fedha zilizotengwa kujenga nyumba za askari jela na polisi Ksh2 bilioni ni pesa chache sana. Haziwezi kugharamia wala kutosheleza mahitaji ya askari wetu. Ikiwa tunataka kupatiwa ulinzi unaofaa, ni lazima tukubali kuwaangalia na kuwasaidia wale ambao wanatoa huo ulinzi. Hizo pesa kiasi cha Ksh2 bilioni ni chache sana ukilinganisha hasa na Kshs8 bilioni ambazo idara ya NSIS imepatiwa. Serikali ingeongeza pesa za kujenga nyumba za askari jela, polisi wa kawaida na polisi wa utawala. Bw. Naibu Spika wa Muda, mambo yalizungumzwa hapa kuhusu utalii. Mimi kama mfanyabiashara najua ni vigumu sana kuwaambia watalii waje Kenya kuwaona wanyama na kuwapiga picha kisha waondoke. Sharti shughuli ya utalii iongezewe mambo mengine. Mimi nikitaka kufunga safari ya kwenda Nakuru kutalii, sitataka kwenda huko kunywa chai tu na kurudi Nairobi. Ningependa kwenda Nakuru kunywa chai na kununua zawadi ambayo itakuwa inanikumbusha namna safari yangu ilivyokuwa. Ni muhimu kutaja kwamba idara ya madini haijazingatiwa hata kidogo. Mimi nimetembea huko Israel. Asilimia 75 ya mapato ya nchi ya Israel inatokana na uuzaji wa madini ambayo Waisraeli hawachimbi. Hali ni hiyo hiyo huko Ujerumani na Marekani. Vile vile nimeona huko Thailand na Hong Kong kwamba watalii wanapenda kuishi vizuri na kununua zawadi. Ingekuwa muhimu kwa Serikali yetu kuzingatia idara ya madini kwa sababu hapo ndipo kuna pesa nyingi za nchi hii. Kuna madini mengi ambayo hainunuliwi na watalii. Madini inapochimbwa na kuwekwa kwenye soko huwa inashindana na madini ya dunia. Madini haitengenezwi kwa mashine wala haipikwi kwenye sufuria. Uuzaji wa madini unaweza kukuza uchumi wa nchi sana hata tupate kujivunia. Ningependa sana kiwango fulani cha pesa kitengwe ili kusaidia idara ya madini ili 1210 PARLIAMENTARY DEBATES June 18, 2008 wananchi wa Kenya waweze kuinua uchumi wao kupitia raslimali walizopatiwa na Mungu. Bw. Naibu Spika wa Muda, tumeambiwa kwamba Serikali imetoa pesa za kujenga shule za upili. Ijapokuwa pesa zimetolewa, isiwe kijumla. Tunataka kujua ni pesa kiasi gani ambacho kimetengewa kila sehemu ya uwakilishi Bungeni kulingana na wingi wa watu. Hii ni kwa sababu kuna sehemu fulani ambazo zina wanafunzi 100,000 ilhali sehemu zingine zina wanafunzi 10,000. Kwa hivyo, tunataka kujua jinsi shule hizi zinajengwa. Je, inategemea wingi wa watu katika kila sehemu ya uwakilishi Bungeni? Ningependa kujua nitapata pesa ngapi katika sehemu ninayowakilisha Bungeni na ni shule ngapi zitajengwa. Tumesikia mambo ya barabara. Imekuwa ni kilio katika nchi hii kwamba sheria kadha wa kadha zibadilishwe ili tuweze kukabiliana na mambo ya rushwa. Miaka 45 imepita tangu tujinyakulie Uhuru. Kisingizio kimekuwa kwamba wajenzi wa barabara wanafanya kazi mbovu ilhali hatua haichukuliwi dhidi yao. Hadi leo hatujasikia hata kontrakta mmoja aliyepelekwa kortini. Ni mdomo tu! Tuache kuhutubiwa! Tukitaka kuhutubiwa tutaenda kanisani. Hapa ni Bunge mahali ambapo tunatunga sheria. Ni lazima sheria izingatiwe. Ikiwa Waziri wa Barabara amegundua kwamba barabara zinajengwa vibaya, basi wanaohusika yafaa watiwe mbaroni na wanyang'anywe hizo kazi. Sisi tunawalipa majaji huko kortini! Ni pesa zetu ambazo zinatumika lakini barabara hazijengwi. Bw. Naibu Spika wa Muda, sisi Wabunge tunachukiwa huko nje. Mimi nilipokuwa nikiomba kura, nilikuwa ninaambiwa, \"Ukifika Bungeni, kitu cha kwanza cha kuangalia ni mshahara mnaolipwa ninyi.\" Juzi, Waziri wa Fedha alitoa mwelekeo wa kutaka kutuweka sisi pamoja na wananchi wengine. Litakuwa jambo lisilofurahisha--- Mimi najua sitakuwa kipenzi cha wengi. Hata hivyo, mimi sikuchaguliwa kuwa kipenzi cha wengi. Ikiwa mwananchi wa kawaida ambaye ananunua soda dukani analipa kodi ama yule mwananchi wa kawaida ambaye anapata mshahara wa Ksh15,000 ama Kshs30,000 analipa kodi, mimi nataka kulipa kodi kabisa bila kuulizwa nitalipa na nani. Kwa hivyo, jambo la kulipa kodi ni jambo la kuweka wananchi pamoja. Tunataka tuishi pamoja ili tusionekana kama sisi---"
}