GET /api/v0.1/hansard/entries/193569/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 193569,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/193569/?format=api",
"text_counter": 31,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwatela",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Education",
"speaker": {
"id": 103,
"legal_name": "Andrew Calist Mwatela",
"slug": "andrew-mwatela"
},
"content": " Mhe. Spika, ningependa kuungana na wenzangu kuomboleza vifo vya wenzetu mhe. Kones na mhe. Laboso. Kifo kimetuibia Wabunge muhimu. Ni Wabunge ambao walijitolea kikamilifu kufanya kazi zao. Bw. Spika, historia ya Bunge letu la nchi hii inaonyesha kwamba kila mwanzo wa Bunge jipya ni lazima tupate mkasa. Sitakuwa nimepotea nikisema ni wakati inapofaa tuelekeze macho 1126 PARLIAMENTARY DEBATES June 11, 2008 yetu kwa Mwenyezi Mungu ili tuombe usalama katika nchi hii. Bw. Spika, ningependa kuungana na wale wanaosema kwamba ni muhimu sana uchunguzi kamilifu ufanyike. Si kwa sababu tunafikira kuwa kuna jambo lolote la hujuma lililofanyika, lakini ili kuhakikisha kuwa ripoti itakayotolewa itatumika kuhakikisha kuwa vyombo vinavyotumika kama ndege vimewekwa katika hali inayoridhisha. Bila shaka kuna kosa lililotokea mahali na likasababisha ndege hiyo kuanguka. Bw. Spika, ninasisitiza kwamba inafaa ripoti za ajali zije Bungeni ili tuweze kuzifuatilia na kuhakikisha kuwa mapendekezo yake yanatekelezwa, ili tuhakikishe kuwa ndege zitakazotumiwa na Wabunge zitakuwa salama. Bw. Spika, kwa niaba ya watu wa Mwatate, ambalo ndilo eneo ninalowakilisha, ninatoa rambirambi zangu kwanza kwa watu wa Bomet na Sotik, and pia kwa Bunge hili la Kumi kwa kuwapoteza Wabunge hawa. Bw. Spika, ninaunga mkono Hoja hii."
}