GET /api/v0.1/hansard/entries/194266/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 194266,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/194266/?format=api",
    "text_counter": 205,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Haji",
    "speaker_title": "The Minister of State for Defence",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": " Nakushukuru, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Leo nimemkumbuka mhe. Wamwere ambaye alikuwa Mbunge wa Subukia. Kiingereza kimezidi sana. Kwa hivyo, nitazungumza kwa Lugha ya Kiswahili. Bw. Naibu Spika, ninaunga mkono Hoja ya leo; kwamba inafaa tupate nafasi ya kurudi nyumbani ili tukae na kushauriana na watu wetu. Tunafaa kushauriana nao na kufanya mipango ya maendeleo. Kwanza, ingawa nimesikia Wabunge wengi wakisema kwamba pesa za CDF yafaa zitumwe, lakini ndugu yangu, mhe. C. Kilonzo, atakubaliana nami kwa sababu tulikuwa katika Kamati ya Bunge ya CDF. Jambo la kwanza ambalo Mbunge wa Kamati ya CDF anahitajika kufanya ni kutenga mradi ambao atatekeleza. Baada ya kufanya hivyo, kuna fomu ambazo unahitajika kujaza. Fomu hizo hupelekwa kwa Kamati ya Kitaifa ya CDF ili pesa zipatikane. Ni kweli kwamba Wabunge wapya katika Bunge hili hawajapata nafasi ya kufanya hivyo. Likizo hii itatusaidia kutenga miradi ambayo tungependa kutekeleza kwa kutumia pesa za CDF. Kwa hivyo, ni lazima tuharakishe ili tuweze kuzitumia pesa hizo kwa njia ambayo inafaa. Bw. Naibu Spika, kama vile mhe. Ojaamong alivyosema, tusiwe wachoyo. Tumepata mshahara na marupurupu mengi tukiwa hapa. Likizo ya wiki tatu itafaa sisi kukaa na watu wetu ili tule kuku, ngamia, mahindi na kadhalika. Si hayo tu. Likizo kama hii itatupa nafasi ya kujua na kuyazingatia matatizo ya wananchi wetu. Ningependa kukana yale ambayo ndugu yangu, mhe. Dkt. Khalwale alisema kuhusu Jeshi letu. Nafikiri ni muhimu kwa Wabunge kusoma sheria za nchi hii. Kuna sheria iliopitishwa na Bunge hili, juu ya kazi ya Jeshi letu. Kazi kubwa ya Jeshi letu ni kulinda mipaka yetu. Ya pili ni kuwasaidia wananchi wetu wakati wo wote wanapohitaji misaada. Ni lazimu tufahamu kuwa shule na hospitali zote ambazo zilikuwa nimefungwa, sasa zimefunguliwa. Jeshi letu pia limekarabati barabara nyingi ili wananchi wetu waweze kusafiri kwa urahisi. Kwa hivyo, si haki kuhujumu kazi ya Jeshi letu. Wananchi watahitaji kuchimbiwa mabwawa na visima. Jeshi letu liko tayari kutekeleza hayo yote. Najua kwamba punde si punde, tutapata vifaa vingi vya kuweza kuwasaidia 1060 PARLIAMENTARY DEBATES May 14, 2008 wananchi. Tunafanya hivyo katika Rift Valley, North Rift, Kaskazini Mashariki, Mashariki na tutaendelea kufanya haya yote kwa nchi yetu tukufu ya Kenya. Bw. Naibu Spika, tukizungumza kuhusu mambo ya Grand Opposition, sijui kama mimi silielewi vizuri jambo hili! Sisi hatujakataa kuwa na upinzani! Ni sheria ambayo inakataza kuwa na mpango kama huo. Lakini hata hivyo, kama wewe ni Back-bencher, ni kitu gani ambacho kinakuzuia kuikosoa Serikali? Ni kitu gani ambacho kinakuzuia kuchokora na kujua mambo yanayofanyika katika Serikali? Sisi ambao tuko hapa tumefungwa miguu na mikono. Hata pahali tulipochaguliwa tumefungwa. Nyinyi ndio wajumbe wetu sasa! Ninyi ambao mko katika Back-Bench ndio wajumbe wetu, mtazungumza kwa niaba yetu na wananchi wa Kenya. Ndugu zangu, tumepitia wakati mgumu sana na tunafaa tujaribu kurudisha nchi yetu pamoja. Pia, tunatakiwa kuzungumza na wananchi wa Kenya ili wakae pamoja kama ndugu na dada. Tusijaribu kutenganisha wale ambao Mungu amewaweka pamoja. Mungu angeweza kuwaleta Wajerumani na Waingereza wakae Kenya, lakini hakufanya hivyo! Alituleta sisi, watu wa makabila na dini mbalimbali. Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono."
}