GET /api/v0.1/hansard/entries/194285/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 194285,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/194285/?format=api",
"text_counter": 224,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwatela",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Education",
"speaker": {
"id": 103,
"legal_name": "Andrew Calist Mwatela",
"slug": "andrew-mwatela"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili nami nitoe maoni yangu kuhusu Hoja hii ya kuahirisha shuguli za Bunge kwa muda mfupi wa majuma matatu. Hata hivyo, kabla sijatoa msimamo wangu kuhusu Hoja hii, ningependa kusema kwamba ni tabia ya Serikali zote humu ulimwenguni kuwa imla, yaani kupenda kutumia nguvu. Bw. Naibu Spika, kwa hivyo, kuhusu Wabunge wenzangu ambao wangetaka kuwa na namna ya kushika breki za Serikali kama ilivyotamkwa hapa, naunga mkono msimamo huo ijapokuwa sijui tuiite hiyo Grand Opposition ama nini. Lakini ni lazima tuwe na namna ya kuhakikisha kuwa Serikali itakuwa inafuatwa karibu karibu ili iweze kufanya vile wananchi wanavyotaka. Kwa hivyo, kuhusu hili jambo la kuwa na upinzani, ni muhimu sana kwa nchi hii. Tunajua kulikuwepo wakati ambapo nchi hii ilikuwa inatawaliwa na chama kimoja. Mambo yalifanywa vibaya mpaka tukaharibu sehemu nyingi za maendeleo ya nchi hii. Kwa hivyo, nawaunga mkono kwamba tuwe na namna ya kuweza kuhakikisha kwamba Serikali ina uoga kidogo katika kufanya mambo. Bw. Naibu Spika, kuhusu hii Hoja ya kuahirisha Bunge, ningependa kuwaomba Wabunge wenzangu waelewe jinsi mhe. Bifwoli ametueleza. Ni muhimu turudi katika mawakilisho yetu ili tuwasikize wananchi hasa kuhusu mambo yao ya maendeleo. Ni kweli kwamba wakati tulikuwa tukiomba kura, tulikuwa tumeainisha mikakati ambayo tulikuwa tunaombea kura. Sasa hivi kunazo kero mbali mbali za wananchi ambazo ni muhimu tuzisikize ili nanyi mje hapa kuhakikisha 1064 PARLIAMENTARY DEBATES May 14, 2008 kwamba Serikali inafanya yale mambo wananchi wamesema. Pili, miradi itakayofadhiliwa na hazina ya CDF ni lazima ijulikane ni miradi gani kabla ya pesa kutoka hazina hii kupelekwa katika mawakilisho. Ni muhimu Mbunge awe kule ili aweze kutambua miradi hiyo kisha ailete miswada katika kamati kuu ndipo pesa zitolewe. Ni muhimu sana kuwa na nafasi hii. Naomba kwamba turidhike. Si ukosefu wa kazi Serikalini tu, bali hii ni namna ya kuwawakilisha watu wetu kikamilifu. Tutakuwa na nafasi ya kurudi kwao. Tutazungumza nao ili tujue ni miradi ipi itafanyika na itagharimu pesa ngapi. Vile vile tuweze kuwasilisha miswada ya miradi hii kwa kamati kuu ndiposa tuwafanyie wananchi vile ambavyo watanufaika. Bw. Naibu Spika, tumeambiwa kwamba kamati nyingine hazijachagua wenyeviti wao. Wangetumia wakati huu sasa kufanya hivyo. Hivi sasa tunapoendelea na shuguli za Bunge, inakuwa ni vigumu kuwa na vikao vya kutosha vya kamati hizo. Ningependa pia kutoa maoni kuwa kamati zote za Bunge zikutane ili zipate kujua namna ambavyo zitaweza kuichunguza Serikali hii. Sharti kamati hizo zikae zote pamoja. Hiyo ni njia mojawapo ya kutusaidia kuiwekea Serikali breki. Kwa hayo machache, ningependa kuunga mkono Hoja hii ya kuahirisha Bunge kwa muda wa wiki tatu."
}