GET /api/v0.1/hansard/entries/194302/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 194302,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/194302/?format=api",
    "text_counter": 241,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Asante, Bw. Naibu Spika. Naunga mkono Hoja hii ya kutuwezesha kwenda nyumbani kwa muda wa mapumziko. Muda huu si wa mapumziko tu, mbali ni wakati wa kukutana na wale ambao walitupatia nafasi ya kuja kwenye Bunge hili la kifahari. Bw. Naibu Spika, kwanza, nataka kutoa shukrani kwa Wabunge na Wakenya wote, ambao waliungana na sisi siku ya Jumatatu ili kuweza kuchanga pesa za kuwasaidia wale ambao walifurushwa kutoka makwao baada ya uchaguzi. Nina furaha kusikia kwamba Bw. Spika aliita Kamukunji ya Wabunge wote. Sikuweko; nilikuwa nimeenda kazi Eldoret, lakini nimeambiwa habari nzuri, kwamba Wabunge wote wamekubali kila mmoja kutoa angalau Kshs50,000 ili Wakenya waweze kusaidika. Nataka kutoa shukrani kwa Wabunge wote kwa kujitolea kimhanga ili Wakenya wote waliofurushwa, popote walipo, waweze kurudia maisha yao ya kawaida na kuishi kama watu wengine. Bw. Naibu Spika, pesa ambazo zimetolewa na wananchi, pamoja na zile ambazo Serikali imepangia, haswa zile ambazo zimezungumziwa hapa, zinatakikana kuja kwa Wizara yetu ili kuwasaidia wale ambao walifurshwa makwao. Kila Shilingi itatumika kwa uhakika, na kwa usawa kuwasaidia wale ambao walipata matatizo. Baadaye, ikiwezekana, kutakuwa na kikao kingine cha Kamukunji ambapo nitakuja niwaeleze Wabunge jinsi hela zao, pamoja na zile ambazo zimetolewa na Serikali na wananchi wengine, zitakuwa zimetumika. Bw. Naibu Spika, huu ni wakati wa kwenda kukutana na watu kule mashinani. Nakumbuka kwamba tulipokuwa katika muhula wa Bunge la Tisa, tulikuwa tukiambiwa kuwa hatuonekani katika sehemu zetu za mawakilisho. Wabunge wengi wapya walichaguliwa kwa kuwa sisi hatukuonekana katika sehemu zetu za mawakilisho. 1068 PARLIAMENTARY DEBATES May 14, 2008 Sasa huu ni wakati ambapo Wabunge wapya na wale wa zamani tunatakikana kurudi mashinani kwenda kuzungumza na watu wetu, ili tujue matatizo yao. Tunajua kwamba ikifika mwezi wa sita Bajeti itasomwa, na tutapewa pesa za CDF. Ni vizuri twende tukutane na wananchi kutoka kitongoji kimoja hadi kingine ili kujua mahitaji yao ni yapi. Bw. Naibu Spika, waheshimiwa Wabunge wengi hapa walitafuta viti vyao kwa kudai kuwa wananchi hawakuhusishwa katika masuala ya hazina ya CDF. Swali ambalo nataka kuwauliza wale wanaopinga Hoja hii ni hili: Je, ni wakati gani watapata muda wa kwenda vitongojini kushauriana na wananchi hasa katika masuala ya hazina ya maendeleo ya mashinani au CDF? Wakati ni sasa! Wiki hizi tatu ambazo tukakazopata, zitaweza kutusaidia kufanya hivyo. Bw. Naibu Spika, nashangaa kusikia Mbunge ambaye eneo lake kutoka kona moja hadi nyingine ni kilomita 600 mraba akisema kuwa yeye huwashughulikia watu wake siku mbili za mwisho wa wiki. Yeye huchukua muda wa siku mbili kufika huko. Je, anapozuru huko mwisho wa wiki, atawezaje kujua matatizo ya watu wake kwa muda wa siku mbili? Bw. Naibu Spika, hatuhitaji kuingiza siasa katika suala hili. Kwa kawaida, kabla Bajeti haijasomwa hapa Bungeni huwa kuna umuhimu wa sisi kurudi kwa watu wetu kuzungumza na wao. Ningependa kuwaeleza Wabunge ambao ni wapya umuhimu wa wao kukaa na wale waliowapatia fursa ya kuja hapa. Ikiwa hawatafanya hivyo, basi mwaka 2012 wataiaga Bunge hili kwa sababu watu wao wanawaangalia. Kuna umuhimu kwa sisi pia kwenda kuzungumza na akina mama kuhusu hazina yao. Kuna zaidi ya Kshs700 milioni katika hazina ya akina mama. Pesa hizi hazijatumiwa na akina mama. Tunahitajika kuwaelimisha akina mama ili waweze kufikia hazina hiyo na kuweza kupata mikopo midogo ili waweze kuendelea na hali zao za maisha. Tunaweza kutumia likizo hii kuyatatua matatizo yaliowapata Wakenya mwanzoni mwa mwaka huu. Tunahitajika kwenda ili tukazungumze nao, haswa na vijana, wazee na viongozi wote kwa jumla, ili tuwaeleze umuhimu wa amani nchini. Bw. Naibu Spika, sina mengi ya kusema isipokuwa kuwaomba wale ambao wanataka kupinga Hoja hii wabadili msimamo wao na kuungana nasi ili tuweze kuzuru mashinani na kufanya kazi pamoja na watu wetu. Kwa wale ambao kwao kuna matatizo, haswa ya watu waliofurushwa kutoka makao yao, ningeomba muda wa kuzuru huko ili tuweze kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kila Mkenya anaishi kwa amani. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}