GET /api/v0.1/hansard/entries/194303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 194303,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/194303/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, nasimama hapa kupinga Hoja hii. Ninaelewa kuwa wengi walioteuliwa katika nyadhifa mbalimbali, kama vile Mawaziri, ni vijana na wanawali. Kwa hiyo, wanahitaji muda wa kuweza kuelewa na kuzingatia shughuli zao za kiofisi. Ni vizuri kujiuliza ni nini tumefanya tangu tuje hapa Bungeni. Ni Hoja na Miswada mingapi ambayo imeletwa hapa Bungeni? Je, tumewatumikia wananchi wetu vilivyo? Sisi tumeleta maswali mengi katika Bunge hili, lakini waheshimiwa Mawaziri wetu wamefanya nini? Bw. Naibu Spika, tunaambiwa kwamba wenzetu wanasema kuwa tunatakiwa kurudi mashinani ili tukazungumze na kushauriana wa wale waliotupatia kibali cha kuja hapa Bungeni. Ni sawa! Lakini tunafanya nini siku ya Ijumaa, Jumamosi, Jumapili na Jumatatu? Tumekuwa watu wa jiji la Nairobi? Kama tumekuwa watu wa jiji hili, basi hatuendi nyumbani! Lakini kama tunaenda nyumbani kila mwisho wa wiki, bila shaka tunawasiliana na wale ambao wametupatia nafasi ya kuwawakilisha hapa Bungeni. Bw. Naibu Spika, jambo lingine ambalo ningependa kuchangia ni kuhusu maafa yaliowakumba watu wetu baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana. Inasemekana kwamba huu ni wakati mwafaka wa kushauriana nao. Je, hatuwezi kulishughulikia huu suala hili nyeti wakati Bunge linapoendelea na shughuli zake? Ni lazima twende likizoni ili tuweze kuyashughulikia mambo haya? Bw. Naibu Spika, tunaambiwa kwamba likizo hii ni muhimu kwa sababu ni mtindo wa May 14, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 1069 Bunge hili kufanya hivyo kabla ya Bajeti. Tunaufuata mtindo huu mpaka lini? Naomba tulifikirie jambo hili kwa makini sana. Tukienda likizoni wakati huu, ninaona kama tutakuwa tunayahepa majukumu yetu. Tunahitaji kuyashughulikia maslahi ya watu wetu katika Bunge hili. Ni mambo gani ambayo Mawaziri wetu wangependa kuwasilisha hapa Bungeni ili tuyashughulikie kwa makini kabla ya Bajeti? Je, tukienda nyumbani leo tutawaambia watu wetu tumewafanyia nini? Tumepitisha miswada miwili hapa Bungeni tangu Januari. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, ninapinga Hajo hii."
}