GET /api/v0.1/hansard/entries/194307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 194307,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/194307/?format=api",
"text_counter": 246,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Gumo",
"speaker_title": "The Minister for Regional Development Authorities",
"speaker": {
"id": 160,
"legal_name": "Fredrick fidelis Omulo Gumo",
"slug": "fred-gumo"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, mimi ninaomba tu! Sijasema kuwa hawajafanya makosa, lakini tukitaka uwiano wa kweli; tukitaka watu wasikilizane na kukaa pamoja, ni lazima tuangalie pande zote mbili. Hata kule Uganda, Rais Museveni ametuma watu kuongea na Bw. Kony ilhali amewaua watu wengi. Tunaongea ili mambo yaishe na nchi itulie kwa sababu kila mtu anataka nchi itulie. Pengine kama hakungekuwa na vita, hakungekuwa na Grand Coalition . Hakuna mtu angelifikiria jambo hilo. Sasa ikiwa watu wengine ambao wako ndani ya Serikali wananyamaza ilhali wale walioumia wakipigana wako ndani, hii inaleta vita vibaya. Hata kuna Wabunge wengine ambao hivi karibuni hawataweza kwenda nyumbani kwa sababu ni lazima tusikizane na tukubaliane. Jambo lingine ni kuwa sisi tukiwa hapa kama Grand Coalition, tuko kama kitu kimoja. Hali hii ilitokea kwa sababu tulitaka kuleta Kenya pamoja, tukae pamoja na tuwasaidie wananchi pamoja. Ni haja yetu sasa, sisi kama Wabunge wa pande zote mbili, tuanze kufanya mikutano pamoja tukiwaeleza wananchi--- Ni lazima tufanye kazi pamoja ili tuonekane kama Serikali moja. Tukianza kuvutana na kuonekana kama bado tuko na tofauti, jambo hili halitatusaidia. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}