GET /api/v0.1/hansard/entries/195503/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 195503,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/195503/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumpongeza Waziri wa Fedha kwa kuweza kupanga kikamilifu hali ya fedha zitakazoweza kutumika kwa muda ulio salia, mpaka mwisho wa mwezi wa Juni. Ningependa tu kusema ya kwamba kwa wale ambao walifurushwa makwao, ningependa kumshukuru Waziri kwa kuhakikisha kuwa pesa hizo ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye hazina tayari ameziweka kwenye mipangilio yake. Tutaweza kuzitumia kikamilifu. Jambo ambalo ningependa kusema ni kuwa katika Wizara zote, zikiwemo zile mpya na zile zimekuwako kwa muda mrefu, tungeomba pia zimsaidie Waziri wa Fedha kutengeneza hesabu zake sawa sawa na kufikia mwaka ujao, tukianza mwezi Julai, aweze kuweka pesa za kutosha kwenye Wizara zote. Ningependekeza kuwa wenzangu wote kwenye Wizara zote nchini, waweze kutumia pesa hizo vizuri ili ziweze kuwasaidia wananchi. Kufikia mwisho wa mwezi wa sita, fedha hizo ziwe zimewafaidi Wakenya. Tunasikia kuwa kuna malalamishi kuhusu zile fedha ambazo zimewekwa na Waziri wa Fedha kwenye Wizara nyingi. Lakini kusema ukweli, sioni faida ya malalamishi hayo kwa sababu ukiangalia muda uliosalia, kutoka sasa hadi mwisho wa mwezi wa sita, ni mchache. Tukiweza kutumia vizuri zile pesa ambazo tumepatiwa, zitawafaidi wananchi. Mara nyingi, ikifika mwisho wa mwezi wa sita, inabidi pesa zirudishwe kwenye hazina ya Wizara ya Fedha ilhali zingewafaa Wakenya. Mimi sina mengi ya kusema, isipokuwa ningependa kumuunga mkono Waziri wa Fedha. Waswahili husema kuwa nyota njema huonekana asubuhi. Ahsante sana."
}