HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 195913,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/195913/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwatela",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Education",
"speaker": {
"id": 103,
"legal_name": "Andrew Calist Mwatela",
"slug": "andrew-mwatela"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ili nichangie Hoja hii. Kwanza ningependa kumpongeza Waziri, mhe. Oparanya kwa kuwasilisha Hoja hii Bungeni kwa wakati unaofaa ili wananchi walioko mashambani waanze kushughulikiwa kupitia Hazina ya Maendeleo katika Mawakilisho (CDF). Ningependa kumweleza Waziri kwamba tunahitaji marekebisho zaidi katika sheria inayosimamia Hazina hii. Kwa mfano, sheria inasema kuwa, kiwango kinachoweza kutumika katika shughuli za usimamizi ni asilimia tatu ya pesa zote zilizotengewa sehemu ya uwakilishi Bungeni. Kiasi cha pesa kinachoweza kutumika kuwalipa wanakamati katika vikao vyao pamoja na wafanyakazi na matumizi yote katika sehemu ya uwakilshi bungeni ambayo imepata Kshs40 milioni, ni Kshs1,200,000. Ukijiuliza ni pesa ngapi zitahitajika kuwalipa wanakamati ikiwa kila mwanakamati analipwa Kshs2,500; ambacho ndicho kiwango kilichowekwa, na kuna vikao viwili kwa kila mwezi, kila mwanakamati atachukua Kshs5,000 kila mwezi. Kwa vile tuna wanakamati 15, hii ni kuonyesha kuwa kila mwezi tutawalipa wanakamati Kshs75,000. Ukichukulia hizo Kshs75,000 mara 12, basi utapata Kshs900,000. Hii ni kuonyesha kwamba ukiwa na matumizi ya pesa kutoka kwa ile asilimia tatu, utabaki na Kshs300,000 tu ambazo utatumia kuwalipa wafanyakazi na kugharamia shughuli nyingine katika ofisi. Hiyo pesa kwa kweli haitoshi kwa sababu, kwa mfano, ukilipa kodi ya nyumba ya Kshs10,000 utalazimika kutumia Kshs120,000 katika mwaka. Halafu tuseme uwalipe wafanyakazi wako Kshs40,000, ambacho si kiwango kikubwa sana, hiyo ni kuonyesha kuwa katika mwaka, utatumia Kshs480,000. Tayari gharama hiyo inapita kile kiwango cha asilimia tatu kilichotajwa ambacho ni Kshs1,200,000. Kwa hivyo, ningependa kumuomba Waziri arekebishe hicho kipengele katika sheria inayotawala Hazina hii ili kiasi hicho cha pesa kiongezwe kutoka asilimia tatu hadi asilimia tano. Hilo likifanyika, tutaweza kugharamia vizuri usimamizi katika maofisi na kamati hizo. Pili, ningependa kumuomba Waziri, jinsi nimewasikia Wabunge wenzangu wakiomba, kuwa kiasi cha asilimia mbili na nusu ya mapato ya nchi ni kidogo mno. Ili kuharakisha maendeleo katika nchi hii, pengine tuanze, kwa haraka, kufikiria namna tutakavyoongeza kiasi hicho cha pesa angaa tufikie asilimia tano na, pengine, baada ya mwaka mwingine, asilimia saba na nusu na tuendelee hivyo kwa miaka mitano. Pengine baadaye tutafikia kiwango cha asilimia kumi na tano. 696 PARLIAMENTARY DEBATES April 24, 2008 Mojawapo ya shida tunazozipata katika kutekeleza shughuli za ujenzi na ukarabati katika miradi inayosimamiwa na Hazina ya CDF ni ushirika ulioko kati ya wahandisi wa wilaya na wasimamizi wa maendeleo katika wilaya (DDOs) pamoja na wahandisi wa maji katika wilaya. Wao hutumia miradi hiyo kujitengenezea pesa kibinafsi. Utakuta kuwa mara nyingi miradi ambayo ingefaa kugharimu, kwa mfano, Kshs1 milioni, kwa ushirika wa watu hao, wanafanya miradi hiyo na kuhakikisha kuwa inagharimu pesa nyingi zaidi. Baadaye, wao hujigawia kiwango fulani cha pesa. Katika sehemu yangu ya Bunge, utakuta mradi mmoja ambao pengine umegharimu Kshs1 milioni na unafanana kamili na mradi mwingine ambao umechukua Kshs2 milioni. Hii ni kuonyesha kwamba kutokana na ule mradi uliochukua Kshs2 milioni, bila shaka hiyo Kshs1 milioni imeingia mifukoni mwa watu fulani. Ningeomba, kwa hayo machache, niunge mkono Hoja hii na mara moja tuweze kupata pesa hizi ziwafikie watu wilayani."
}