GET /api/v0.1/hansard/entries/196039/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 196039,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/196039/?format=api",
    "text_counter": 92,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Rai",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Lands",
    "speaker": {
        "id": 203,
        "legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
        "slug": "samuel-rai"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba pia niungane na wenzangu ambao wamekata shauri kuiunga Hoja hii mkono. Bw. Naibu Spika wa Muda, nataka kwanza kumshukuru Bw. Ethuro kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili. Mimi nawakilisha watu katika sehemu za mashambani. Ni jambo la kusikitisha kwamba watu hao wameteseka kwa sababu ya mambo haya ya vitambulisho kwa muda mrefu. Kama tungekata shauri kwa kauli moja kuipitisha Hoja hii, labda tungepunguza ule msongamano wa matatizo yanayowakumba watu wetu. Utakuta kwamba kuna baadhi ya watu ambao wamefika umri wa kuolewa na wanakaa mpaka wanazaa watoto wakiwa bado hawajapata vitambulisha, kwa sababu ya yale masharti ya kupata vitambulisho pekee yake. Kwa hivyo, tungeweza kukata shauri na kusema kwamba kitambulisho kinaweza kutumika na kufanya kazi zote mbili, nafikiri tutakuwa tumepunguza msongamano, kazi nyingi na pia hata gharama. Lakini, utakuta kwamba ni swala la Serikali kufikiria umuhimu wa Hoja hii kuletwa katika Bunge hili. Tusipofikiria kwamba mambo mengine tunayafanya yanatuongezea gharama sisi wenyewe, itakuwa ni hasara kwa nchi hii vile vile. Bw. Naibu Spika wa Muda, Hoja hii imekuja kwa wakati ambapo tunahitaji kuweka maanani na kujua kwamba, katika kusambaza vitambulisho katika sehemu za kule mashambani, maofisa wa usajili wa watu wawekwe katika Wilaya. Wakati huu, tungefikiria kwamba maofisa hao wawekwe katika kata dogo zetu. Wanafaa kuwa pale kutoka Janauri mpaka Desemba wakifanya kazi ya kupeana vitambulisho kwa watu wetu. Ni swala la kusikitisha kwamba mtu anaweza kuchukua zaidi ya miezi sita kupata kitambulisho, ilhali ni mtu amezaliwa mahali fulani na anajulikana kwa majina. Lakini kama vile Bw. Naibu wa Spika alisema, kwa sababu ya majina peke yake, inakuwa ni swala la kuambiwa kwamba eti kuna kitu kinaitwa vetting . Sasa mtu amezaliwa hapo na anajulikana kwamba ni Mkenya--- Lakini utashangaa Bw. Artur Margaryan alipokuja hapa, hakufika katika Wizara ya Uhamiaji na Usajili wa Watu. Lakini alipata pasipoti. Hilo liliwezekana. Lakini kwa Mkenya April 23, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 603 kupata kitambulisho ambacho kinajulikana kwamba ni haki yake na kinaweza kumsaidia yeye kufanya mambo yake na kujisadia kwa mambo mengi tofauti tofauti, inakuwa ni kazi ngumu. Huwezi kufanya jambo lolote, kuuza au kunua chochote wakati huu bila kitambulisho na PersonalIdentification Number (PIN) . Hili swala la kusema kwamba ni lazima eti uwe na kadi ya uchaguzi ni ya maana gani? Nambari ya kitambulisho inakupa usahihisho kwamba wewe ni Mkenya na unastahili kupiga kura. Hii kadi nyingine ya pili ni ya kazi gani? Haya yote ni watu kujiongezea mambo ili wapate kujinufaisha. Ndiposa unakuta kwamba, mara kwa mara, unaambiwa pasipoti zimeagizwa kutoka nje ilhali watu wamekula pesa. Vitambulisho havipatikani! Vimeagizwa kutoka nje lakini watu wamekula pesa. Mpaka lini mambo haya yataendelea? Utaambiwa kwamba watu wamekuja kutoka wilayani ili kuwasajili watu. Lakini inawachukua mwendo mrefu kufika katika lokesheni. Watafanya kazi masaa matatu peke yake. Sasa, utakuta kwamba inapofika wakati wa uchaguzi, kuna msongamano wa watu wanaotaka kuchukua vitambulisho na haiwezekani! Bw. Naibu Spika wa Muda, wakati mwingine, kwa sababu ya kutojua, watu wetu hawatilii maanani kwamba kuna umuhimu wa kuchukua vitambulisho. Wakati mwingine mtu hukata shauri na kusema: \"Kuna haja gani ya kuwa na kitambulisho? Ninajulikana mimi ni Mkenya; wacha niishi tu!\" Mtu kama huyo atakaa hivi mpaka alazimike kuwa na kitambulisho. Sheria inazidi kuongeza masharti kwa kusema kwamba ni lazima mtu huyo aende akachukue hati ya kiapo. Hii inamaniisha ni lazima atoke kwake aende mahakamani. Mtu kama huyo hajui mambo ya mahakamani. Ukimtajia mahakamani, ataona kwamba ni mahali ambapo panashtakiwa watu. Mambo yakifika kiwango hiki anasema: \"Nimeachana na mambo haya\". Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba Wizara iwasaidie watu wetu ili, kwanza, wapate kujua njia rahisi ya kupata vyeti vya kuzaliwa, hasa wale ambao hawakujaliwa kujifungua hospitalini. Tumekuwa tukijenga zahanati katika location zetu ili watu wapate kujifungua katika zahanati hizo. Tumejenga zahanati nyingi na hakuna wafanyakazi wa kutosha. Sasa, tutazipata kwa njia gani karatasi za notification of birth ? Imekuwa ni shida kupata cheti cha kuzaliwa na kujua miaka. Mtu anaambiwa akitaka kitambulisho ni lazima umri wako ukadiriwe. Eti mtu akakuhesabu meno ili ajue miaka yako ni mingapi! Hayo yatakuingia akilini? Hata DO akiwa pale anaweza kukuhesabu meno ili ajue una miaka mingapi! Pia unaweza kuambiwa uende kwa daktari. Daktari naye anahitaji senti. Ukitoka hapo unaambiwa uende kortini. Huko unahitaji Kshs1,500 za hati ya kiapo. Ni nani atagharamia mambo hayo yote? Bw. Naibu Spika wa Muda, kazi yetu kubwa ni kusema kwamba vitu ni vya bure. Tunasema tumepunguza hiki na kile. Lakini mzigo unautoa kichwani unauweka begani. Hujamsaidia mwananchi ukifanya hivyo! Bado angali na shida. Wakati umefika kwa Hoja hii kupitishwa kwa kauli moja, na Serikali ikimbie kwa haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha kwamba Hoja hii imekuwa Sheria ili watu kule mashinani waanze kupata vitambulisho. Wakati wa kupiga kura utakapofika, hatutaanza kukimbizana tukitafuta kadi za kura. Hoja hii ikipita mtu ataweza kutumia kitambulisho peke yake kupiga kura. Namba ya kitambulisho itatosha. Mtu hawezi kuwa na namba mbili. Mambo ulimwenguni yamebadilika na ni lazima pia tubadilike. Tusipobadilika mtu atatakiwa kuwa na kitambulisho, kadi ya kupiga kura, beji na juu yake picha. Mambo kama haya hayatatusaidia. Haja yetu kubwa ni kuchagua viongozi. Katika nchi yetu kuna watu wasio na kadi za kura na hawawezi kupiga kura ingawa wamehitimu umri wa kupiga kura. Hii ni kwa sababu kadi za kura hazikuweza kupatikana kwa wakati uliofaa. Bw. Naibu Spika wa Muda, naona wakati wangu umekaribia kuisha, na ningependa kumshukuru mwenye kuileta Hoja hii. Naomba sote tuiunge mkono kwa umoja ili Waziri aitilie maanani, na ajue kwamba Hoja hii itakuwa na manufaa kwa taifa hili. Namwomba Waziri atambue kwamba kuna umuhimu wa kuwatoa maofisa wanaofanya kazi katika sehemu za wilaya, na kuwapeleka mashinani ili bei ya usafiri ipungue. Kuwalazimisha watu wetu wakati wote kusafiri si 604 PARLIAMENTARY DEBATES April 23, 2008 vizuri. Wakati mwingine watu huambiwa kwamba gari inayowasafirisha maofisa wa kutoa vitambulisho haina mafuta. Twataka Mbunge akaitie mafuta ndipo iende ikafanye kazi? Kesho ataambiwa kwamba maofisa hawana marupurupu. Itakuwa kazi ya Mbunge kuwatafutia maofisa hawa marupurupu ili wafanye kazi? Bajeti inaletwa hapa ya kazi gani? Itakuwa tunafanya kazi duni ambayo haieleweki. Wakati mwingine hatuna majibu ya kuwapa wananchi, kwa sababu ukiwambia kwamba gari inayowasafirisha maofisa wa kutoa vitambulisho haina mafuta, ni kama kumpigia mbuzi guitar, kwa sababu hataelewa unamwambia kitu gani. Serikali imetenga pesa za kununua mafuta ya gari za Wizara. Wizara nayo yasema haikutengewa pesa za kununua mafuta. Sasa, tutauliza nani maswali? Bw. Naibu Spika wa Muda, safari hii Wizara imepata mwenyewe. Tuna matarajio makubwa, kwa sababu Waziri alisema kwamba alipopata habari za kuteuliwa kwake alikuwa anapumzika, na hakutarajia kwamba angeteuliwa katika Wizara hii. Watu wengi huenda katika Wizara wakiwa na kusudi tu la kutengeneza pesa. Siamini kwamba Waziri huyu ameenda kutengeneza pesa. Alitengeneza pesa alipokuwa wakili. Sasa ameenda kufanya kazi. Tunatarajia kuona mabadiliko makubwa katika Wizara yake. Pia tunataka kuona msongamano wa watu ukipungua katika ofisi za Wizara hii. Tunataka kuona matatizo yanayowakumba maofisa mashinani yakipungua. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache, na unga mkono Hoja hii."
}