GET /api/v0.1/hansard/entries/196041/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 196041,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/196041/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Ahsante sana Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili nami nichangie kwenye mjadala huu wa leo ambao ni muhimu sana. Ningependa kumshukuru mhe. Ethuro kwa kuleta Hoja hii ambayo ni muhimu sana. Jambo hili la kuunganisha kadi hizi mbili ni muhimu sana kwa sababu kadi ya kupiga kura hutumika wakati mmoja tu baada ya miaka mitano. Ni jambo gumu mno kuiweka kadi hiyo katika hali inayofaa. Kadi hizi zinamilikiwa hata na watu walioko mashinani, hasa mashambani, ambao hawazingatii namna ya kuziweka. Kwa sababu ni kitu ambacho kinatumika mara moja baada ya muda mrefu, ni rahisi sana kukipoteza. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha kuona kwamba baada ya watu kuhimizwa wajiandikishe ili wapige kura, wanasiasa fulani wamechukua nafasi hiyo kuwazuia watu fulani ambao hawawaungi mkono. Mara nyingi huwa wanawaendea makarani wanaoandikisha watu na kuwaambia watoe majina ya watu fulani. Huwa ni orodha ndefu lakini yule mtu akifika pale kujiandikisha, kwa sababu kile kitambulisho chake hakiwezi kutumika kupiga kura, anashurutishwa kurudi kwake yule karani aliyemsajili, tuseme, mara kumi. Yule mtu akirudi mara ya 11, atalazimishwa kutoa hongo. Utoaji hongo ni tabia ambayo kila Mbunge na kila mwananchi wa Kenya amejitoa mhanga kupigana nayo ili tuitoe katika fikira za Wakenya kabisa. Kitambulisho kimeletwa na mkoloni na kimetumiwa kututusi sisi Wakenya. Mtu anaposajiliwa ili apate kitambulisho, yeye huulizwa eti ni wa kabila gani na anatoka wapi. Kinachobaki sasa ni mtu kuulizwa: \"Kwa nini ulizaliwa Mkikuyu, Mkamba au Mkalenjin?\" Hilo ni jambo la kuudhi sana! Utakuta kwamba ikiwa kuna mtu amezaliwa katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki na angependa kujiandikisha katika Mkoa wa Nyanza, kuna maswali huyo mtu ataulizwa, kwa mfano: \"Kwa nini wewe asilia yako ni ya Kisomali ama Kiturkana?\" Mara nyingine watu huulizwa: \"Kwa nini unakuja kujiandikisha hapa Kisumu?\" Huyo mtu ataulizwa hayo maswali ilhali yeye hulipa kodi yake kwa Serikali na pesa hizo zinatumika katika kunafaisha Kenya nzima. Wakati mtu analipa hiyo kodi, haulizwi kwa nini anailipia mahali pale ambako hakuzaliwa! Bw. Naibu Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha sana kwamba baada ya kupewa kitambulisho na mkoloni, tumeongezewa stakabadhi nyingine iitwayo Passport . Hii Passport inatolewa katika sehemu zilizochaguliwa kwa mapenzi ya watu fulani. Utakuta kwamba yule 606 PARLIAMENTARY DEBATES April 23, 2008 Maasai ambaye amezaliwa Mkoa wa Bonde la Ufa na ni mkaazi wa Kajiado, analazimika kuja kuchukuwa Passport yake hapa Nairobi. Nauli ya kutoka anakokaa hadi hapa Nairobi ni Kshs400. Yule karani anayeshughulikia Passport ya huyo mtu--- Ningependa Bw. Mapambano, Waziri mwenyewe asikie. Yule mtu kutoka Kajiado akionekana, atalazimishwa kusafiri kila mara kuja Nairobi kutafuta hiyo Passport . Mwishowe, ataambiwa ikiwa anataka kukatiza gharama yake ya usafiri na kujipunguzia hasara, basi apeane hongo ya Kshs10,000. Huyo mtu anakosa la kufanya hasa akifikiria safari alizofanya kutoka Kajiado hadi Nairobi ambazo zimemgharimu kiasi cha pesa Kshs4,000. Pengine ameuza ng'ombe wake ili apate pesa za kuhongana ili apate Passport."
}