GET /api/v0.1/hansard/entries/196045/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 196045,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/196045/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "zipeanwe katika sehemu moja ya nchi hii. Tunataka zisambazwe kwa sababu katika kila mkoa na kata kuna wawakilishi wa Serikali. Watumishi wa Serikali ambao hawawezi kuaminika wafutwe kazi na wanaoaminika wapewe kazi hiyo. Matusi yamekuwa mengi kwa sababu unapewa kitambulisho na tena unaenda kutafuta kadi ya kupiga kura. Sisi kama wananchi na Wabunge katika Bunge hili tungependa kusema kwamba ni jambo la maana sana kuhakikisha kwamba kile kitambulisho tuliachiwa na Mkoloni--- Serikali imeleta kadi nyingine ya kupiga kura. Kwa hivyo, tutumie kitambulisho hicho hicho kupiga kura. Tusiwe na kadi mbili. Aidha, wakati wa kujiandikisha kura huwa inasingiziwa eti zile kadi zilizotumika katika kupiga kura wakati uliopita hazifai na sharti zibadilishwe. Mwenye kutoa wazo hilo huwa anatafuta hela katika Serikali. Yeye atachukua kile kikaratasi na kukifanyia mabadiliko madogo tu. Kwa mfano, atakikata tu kwenye upande mmoja ili ionekane kwamba kadi hiyo imebadilishwa. Pesa zinazolipishwa kufanya hiyo kazi ni maradufu ya zile zingetumika kihalali. Mhe. Shakeel ameongea hapa kuhusu amani. Tunataka amani iingie Kenya. Ni matumaini yetu sisi kama viongozi kukaa kando na kuzungumzia maswala ya kikabila. Juzi, Serikali iliundwa na Mawaziri ambao ni watoto wa nchi hii wakachaguliwa. Wao wamefuzu na wana stakabadhi zao. Hata hivyo, bado sisi tunatoa maagizo huko nje na kusema kwamba sisi hatukupewa haki yetu. Haki ya Waziri kukaa katika ofisi siyo kupeleka ile bendera nyumbani kwake, katika Wakilisho lake au kwa jamii yake. Ile bendera ni ya kutoa utumishi kwa wananchi wa Kenya. Tusiendelee kufikiria kwamba utumishi kwa umma utawekwa kulingana na mahali ambako mtu amezaliwa. Ikiwa wewe unatoka sehemu fulani na watu wa sehemu hiyo wana vyeo, si lazima wewe ufaidike. Ikiwa kuna Waziri anayetumia Wizara yake kuwafaidi watu wa sehemu fulani, basi bendera hiyo ipewe mtu mwingine ambaye atawatumikia wananchi wote bila mapendeleo. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}