GET /api/v0.1/hansard/entries/196975/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 196975,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/196975/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Rai",
    "speaker_title": "The Member for Kinango",
    "speaker": {
        "id": 203,
        "legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
        "slug": "samuel-rai"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ninakupongeza kwa kunipa nafasi hii ili nitoe mchango wangu juu ya Hotuba ya mhe. Rais. Kwanza nataka kuwashukuru watu wa Kinango kwa kunichagua tena kwa kipindi cha tatu. Hii ni heshima kubwa kwangu. Nataka niwaahidi hapa kwamba nitafanya kila niwezalo ili kuona kwamba nitawatumikia vilivyo. Bw. Naibu Spika, nawapongeza waheshimiwa Wabunge wenzangu waliochaguliwa kujiunga na Bunge hili la Kumi. Nataka nichukue nafasi hii pia nikupongeze wewe kwa kuchaguliwa kuwa Naibu wa Spika. Hotuba ya Mheshimiwa Rais ilitupa kielelezo mwafaka katika hali ya kuweza kuliongoza taifa hili."
}