GET /api/v0.1/hansard/entries/196978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 196978,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/196978/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Rai",
    "speaker_title": "The Member for Kinango",
    "speaker": {
        "id": 203,
        "legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
        "slug": "samuel-rai"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika, sitaki kumjibu Bw. Kajembe kwa sababu ana sababu nyingi za kufanya hivyo. Bw. Naibu Spika, nataka nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutupa sisi kielelezo katika Hotuba yake. Jambo ambalo ningependa kulisisitiza ni kwamba kwa muda wa miaka 44 ya Uhuru, sisi Wakenya tunaweza kujilaumu kwa hali mbaya hapa nchini. Kwa muda huu wote tumekuwa na Serikali na Mawaziri. Hata hivyo, ubinafsi umefanya kazi kwa muda mrefu kiasi cha kwamba ni vigumu kuweza kuyaona matokeo ya kazi nzuri ya kuwa na Serikali kwa muda huu wote. Hii ni kwa sababu kila anayechaguliwa kuwa na mamlaka hufikiria njia za kujinufaisha mwenyewe. Bw. Naibu Spika, kuna wakati Mawaziri wengi hapa nchini hawakufanya kazi zao vilivyo. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuandamana na mhe. Rais pahala pote alikozuru. Walikuwa wakifanya hivyo, ili kuthibitisha imani yao kwake na kuwaacha wananchi wetu wakiteseka. Jambo hilo liliwaumiza Wakenya kwa muda mrefu. Ningependa kutoa shukrani kwa sababu kila baa lina heri lake. Shida iliyotupata juzi baada ya uchaguzi ilikuwa na heri yake. Ni mara ya kwanza katika taifa hii kuwa na Waziri Mkuu ambaye atakuwa na jukumu la kuhakikisha kwamba kazi ya Mawaziri inafanyika. Mawaziri hawa bila mnyapara hawawezi kufanya kazi. Nina imani kwamba tukiwa na mnyapara ambaye atakuwa 378 PARLIAMENTARY DEBATES March 25, 2008 akiangalia kazi yao, kazi itafanyika vizuri. Ikiwa hawatafanya kazi vizuri, basi wataonyeshwa njia ya kurudi nyumbani. Tutaona tofauti kubwa sana."
}