GET /api/v0.1/hansard/entries/196980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 196980,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/196980/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Rai",
"speaker_title": "The Member for Kinango",
"speaker": {
"id": 203,
"legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
"slug": "samuel-rai"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, sitaki kumjibu kwa sababu hayo ni maoni yake. Ninataka afahamu kwamba kumewekwa mtu ambaye atakuwa anasimamia kazi ya watu fulani na basi huyu ni mnyapara. Yeye anaangalia kazi za watu wengine na kuhakikisha kwamba zinafanywa vizuri. Kama mhe. Mbunge hajui Lugha ya Kiswahili, basi atajifundisha muda atakapokuwa katika Bunge hili. Bw. Naibu Spika, wakati Waziri Mkuu mtarajiwa atakapoanza kazi yake, mhesimiwa Mbunge atajua kazi yake ni ipi. Kuna tofauti kati ya mawaziri na Waziri Mkuu ambaye atakuwa akifanya kazi katika Bunge hili. Mawaziri watakuwa wanajua kwamba wanafanya kazi zao lakini kuna mtu ambaye baadaye anaangalia kazi hizo zinafanyika kwa njia gani. Pia wananchi watakuwa na njia ya kutoa malalamishi yao kama kazi haitakuwa imefanyika vizuri. Wananchi na viongozi wakipewa nafasi kama hii, basi ninaamini kwamba kazi itafanyika na matokeo yatapatikana. Tunahitaji maendeleo. Bw. Naibu Spika, ninawakilisha sehemu ya Kinango. Uhuru ulipatikana siku moja; bendera ikapandishwa na ikaeleweka kwamba Kenya imejipatia Uhuru. Jambo la kushangaza ni kwamba katika pembe mbali mbali za Jamhuri hii kuna tofauti fulani za kimaendeleo. Hadi kufikia hivi sasa, kuna baadhi ya watu fulani ambao wanaishi katika maisha ya umaskini zaidi kuliko wengine. Hili ni jambo la kusikitisha. Ni lazima tufahamu kwamba kama ni jambo la kugawanya raslimali, itakuwaje sehemu fulani kuwa na barabara kumi za lami na kwingine hata barabara moja hakuna? Ni jambo la kusikitisha. Tunaiomba Serikali iangazie sehemu za mashambani na kuona kwamba kuna mawasiliano mazuri. Ninakumbuka mwaka jana, mwezi wa nane, Rais wa Jamhuri alizuru sehemu yangu na akatoa amri kwamba barabara ya kutoka Kwale kuelekea Kinango itiwe lami. Mpaka sasa, sijasikia wala kuona lolote likifanyika. Alitoa pia amri kwamba walimu 50 waajiriwe, lakini Waziri mhusika wakati huo ni kama aliyaweka masikio yake pamba. Mpaka sasa, hao walimu hawajawahi kuajiriwa. Kinachohitajika ilikuwa ni yeye kuandika barua ya kusema waajiriwe. Jambo hilo pekee lilimshinda. Bw. Naibu Spika, hospitali ya Kinango ilipandishwa cheo na kuwa hospitali ya wilaya. Jambo la kusikitisha ni kwamba baadhi ya vifaa havifanyi kazi. Hata chumba cha kuhifadhia maiti hakina maji ya kutosha. Wiki tatu zinaweza kupita bila maji kupatikana huko Kinango. Chumba cha kuhifadhia maiti kinahitaji maji ya kutosha ili kipate kujiendeleza. Mambo kama haya ni lazima yatiliwe maanani. Ikiwa mtu atafariki akiwa Kinango, basi atahitajika kuchukuliwa hadi Msambweni. Tunajua kuipeleka maiti kutoka Kinango hadi Msambweni ni kama kumwaadhibu. Jambo kama hili ni lazima liangaliwe kwa makini. Tunahitaji pipa la maji ambalo litatosheleza mahitaji yetu. Tunataka kuona hospitali yetu ikiendesha mipango yake. Bw. Naibu Spika, tuliahidiwa umeme kutoka Mariakani kupitia Samburu, Taru hadi Mackinon. Tuliambiwa ya kwamba Serikali ya Ufaransa ingesambaza umeme kwa gharama ya Kshs95 milioni. Hadi kufikia hivi sasa ni zaidi ya karibu mwaka moja na nusu na umeme huo hatujauona. Watu wetu wamejiandikisha na wengi wamelipa pesa ili wapate umeme huo. Hawajui wataupata umeme huo lini. Hili ni jambo ambalo linatusikitisha. Kwa hivyo, tunaomba tufunguliwe barabara yetu. Pia tunaomba maslahi yetu ya maji yaangaliwe kwa sababu kufikia hivi sasa tuna mfreji unaopeleka maji sehemu za Vigurungani. Kwa sababu ya umaskini, tunaomba Serikali iwapatie tu vyakula wananchi ambao wanachimba mtaro wa kuweka mifereji ya maji. March 25, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 379 Kwa sababu ya hali ya njaa, ni vigumu mwananchi kushinda akichimba mtaro na hatimaye jioni hana chakula. Hilo ni tatizo ngumu. Bwana Naibu Spika, sisi, kama wananchi wengine, tunahitaji huduma za Serikali. Tuliomba kifaa cha kutuwezesha kupiga simu za STD lakini hadi kufikia hivi sasa Kinango haina kifaa kama hicho. Tunaomba tupatiwe kifaa hicho ili tuweze kuingia katika mtandao, yaani,"
}