GET /api/v0.1/hansard/entries/197174/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 197174,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/197174/?format=api",
    "text_counter": 62,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwakwere",
    "speaker_title": "The Minister for Transport",
    "speaker": {
        "id": 189,
        "legal_name": "Chirau Ali Mwakwere",
        "slug": "chirau-mwakwere"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, na ndugu zangu Wabunge, kwanza nataka kutoa shukrani kwenu nyote kwa kumchagua mhe. Marende kuwa Spika wetu na kinara wa Bunge hili la Kumi la Jamhuri ya Kenya. Hatukufanya makosa na amedhihirisha kweli kuwa anaweza kusimamia utaratibu wa Bunge kwa hizi siku chache ambazo amekalia Kiti hicho. Tunampongeza sana kwa uhodari wake aliotuonyesha. Pili, nataka kumsifu Rais Kibaki. Nimesimama kuunga mkono hii Hoja ambayo iko mbele yetu. Rais Kibaki alitoa mwongozo ambao sisi kama Wakenya tukiufuata, basi tutasonga mbele kimaendeleo katika hali ya kutufurahisha na nchi zote duniani zitajua kuwa Kenya ipo. Rais Kibaki alitugusia kule tulikotoka na akatukumbusha pale tulipo. Alitusihi tujitayarishe kuifanya Kenya iwe bora kwa miaka ijayo ili iwe na manufaa kwetu sisi na vizazi vyote vijavyo. Huu ndio wajibu wetu kama Wabunge. Ni wajibu wetu na ni kazi ambayo tutaweza kuifanya. Tumeianza kazi hiyo kwa mfano ambao umetolewa na viongozi wa vyama vikubwa. Uongozi ambao Rais Kibaki pamoja na mhe. Raila walionyesha ni hali ambayo kwa hakika, imeturidhisha sisi sote. Tunajua kwamba tuna mwanzo ambao utaleta manufaa makubwa nchini. Bw. Naibu Spika wa Muda, madhumuni ya chama chochote kile cha kisiasa ni kuunda Serikali. Hata madhumuni ya Chama cha Shirikisho ilikuwa ni kuunda Serikali. Ikiwa madhumuni ni kuunda Serikali na viongozi wa vyama wamekuja pamoja ili waunde Serikali, basi hilo ni jambo la busara kwa sababu limetuleta sisi pamoja. Nakumbuka Rais Kibaki akituambia kuwa watoto wetu, kokote wanakosoma, wako pamoja wala hawazungumzi mambo ya ukabila au utengano wowote. Wao wanajichukulia kama Wakenya. Sisi, tulivyofanya hapa yaani kuja pamoja kuunda Serikali, ni kama tumefundishwa na watoto wetu kuwa lazima tuwe kitu kimoja na tusitengane ili tuweze kupata manufaa ya maendeleo hapa Kenya. Kwa hivyo, tunawashukuru watoto wetu. Mara nyingine ni vizuri kuiga wanavyofanya watoto wetu ili nchi nzima isonge mbele. Bw. Naibu Spika wa Muda, madhumuni ya chama chochote ni kuunda Serikali. Kwa nini tunaunda Serikali? Kuunda Serikali ni kuhakikisha kwamba uchumi na hali ya maisha ya wananchi 330 PARLIAMENTARY DEBATES March 20, 2008 inazidi kuwa bora kila wakati. Inaweza kuwa bora kwa sababu kuna sehemu za maendeleo ambazo ni muhimu tuziangalie sawa sawa. Kwa mfano; ikiwa ni usalama, tunaunda Serikali ili tuwe na usalama thabiti. Tunaunda Serikali tuwe na usalama ili tuweze kufanya mambo mengine ya kuendeleza nchi bila wasiwasi au woga. Kuja pamoja kwa viongozi wetu ni mfano mzuri. Sote Wabunge tuje pamoja sawa sawa na pale ambapo kuna makosa, basi tutoe maoni yetu juu ya makosa hayo. Mara nyingi kuna ukweli wa yale tunaambiwa ama tunayotaka kufanya. Basi tuungane pamoja ili tuweze kuleta maendeleo na usalama katika nchi yetu. Yaliyopita si ndwele; tugange yajayo. Juzi na jana tuliumizana. Ni ishara kwamba baada ya kila uchaguzi, wananchi katika sehemu fulani za nchi huanzisha vurugu. Wao si kwamba hupigana kwa kuwa kuna matokeo ya uchaguzi yasiyoridhisha, bali huwa wanakumbuka yale maonevu na dhuluma walizopata miaka mingi iliyopita hata zama za wakoloni. Watu wengine husahau kuwa kila mwaka watu wa Matuga, baada ya uchaguzi, hujitolea kupigania haki zao. Wengi wamesikia Kaya Bombo. Kaya Bombo iko Matuga, ambalo ndilo wakilisho langu. Tulikuwa tukipigana kila baada ya uchaguzi kwa sababu tulikuwa tunakumbuka dhuluma tulizopata miaka mingi iliyopita kuhusu mambo ya mashamba. Sisi tulifanywa maskwota kutoka wakati wa ukoloni. Tuliibiwa, tulinyang'anywa, tulinyimwa, tulitukanwa na tukadharauliwa. Watu wetu hukumbuka mambo hayo yote baada ya uchaguzi kwa sababu ni hali ambayo kila mmoja huzungumza na mwingine. Tunafahamu kuwa watu wanaishi pamoja. Tulipigana vita mwaka wa 1992 lakini ardhi yetu hatukupata. Mwaka wa 1997 baada ya uchaguzi tukang'ang'ana katika vita tena, lakini hatukupata ardhi yetu. Naishukuru sana Serikali ya Rais Kibaki kwa sababu katika miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake, sisi watu wa Mkoa wa Pwani ambao wengi wetu ni maskwota, aliamua kwamba Serikali itaweka utaratibu ili kuwepo na mashamba ili awagawie wananchi ndiposa waweze kuwa na ardhi. Kazi hiyo imeanza lakini haijamalizika. Hii ndiyo sababu kubwa kabisa ambayo watu wa Matuga na Wapwani wote hawakupigana tena baada ya uchaguzi wa hivi majuzi. Serikali imeanza kutekeleza utaratibu huo na mashamba yameanza kununuliwa. Wananchi wameanza kugawanyiwa mashamba sawa sawa. Hiyo imeleta amani. Je, nasema hivyo kwa nini? Ni kwa sababu yale yote tumeona sharti tuyaangalie sawa sawa. Ni lazima tuhakikishe kuwa wananchi wamepata haki zao. Bw. Naibu Spika wa Muda, utaratibu unaweza kufanyika kwa sababu tumekuja pamoja na hakuna anayetupinga. Hakuna upinzani. Kazi ya chama cha upinzani ni kupinga lolote linalosemwa na Serikali, liwe bora au baya. Sasa tumevuka msimu huo. Tuko pamoja na ni lazima tuchukue msimamo ambao utaondoa shida za wenzetu ambao wamepigana, si kwa sababu ya matokeo ya uchaguzi au matamshi kuhusu mshindi au aliyeshindwa, bali ni kwa sababu ya kukumbuka zile shida walizopata miaka mingi iliyopita. Lolote huweza kutokea wakati kama huo kwa sababu watu huwa wako pamoja. Sisi kama nchi tumesonga mbele kiuchumi. Uchumi wetu unasonga mbele vilivyo kwa sababu ya uongozi ambao Rais Kibaki ameleta."
}