GET /api/v0.1/hansard/entries/197177/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 197177,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/197177/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwakwere",
"speaker_title": "The Minister for Transport",
"speaker": {
"id": 189,
"legal_name": "Chirau Ali Mwakwere",
"slug": "chirau-mwakwere"
},
"content": " Nakushukuru sana Bw. Naibu Spika wa March 20, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 331 Muda. Labda hakunielewa kwa sababu nimeongea kwa lugha ya Kiswahili. Lakini kimombo nakijua sawa sawa. Nikianza kukisakata labda atanielewa sawa sawa. Lakini kwa vile sheria zetu zinasema kuwa ukianza kuzungumza kwa lugha moja sharti uendelee nayo hadi mwisho, sitamweleza kwa Kiingereza. Nitafanya hivyo tukishatoka nje na labda atanielewa sawasawa. Huu ni wakati wa kihistoria kwa Kenya nzima. Ni historia kwa sababu mambo hayajawahi kuwa hivi. Zamani tulikuwa pamoja kabisa lakini katika Katiba ambayo ilikuwa inaruhusu chama kimoja cha kisiasa. Hali hii ni tofauti. Tusichukuliwe eti tumerudi nyuma; la, hasha, tumesonga mbele. Hii ni kwa sababu wakati ule tulikuwa na chama kimoja cha kisiasa. Fikira zetu wakati huo zilikuwa juu ya chama tu, lakini sasa tunafikiria maendeleo. Hayo ndiyo madhumuni yetu makubwa ya kuja pamoja. Tunataka maendeleo katika nchi yetu. Bw. Naibu Spika wa Muda, naishukuru sana Serikali ya miaka mitano ya kwanza ya Rais Kibaki kwa kukuza uchumi kutoka takwimu iliyokuwa dhaifu sana hadi asilimia saba kwa mwaka. Huu ni ushindi mkubwa na dunia nzima inajua hivyo. Labda ndiyo sababu dunia nzima ilipoona sisi wenyewe hatuelewani, walikuja hapa kuhakikisha kwamba tunaelewana ili tuwe mfano kwa dunia nzima. Sisi Wakenya ni mfano kwa dunia nzima. Labda sisi wenyewe hatujui hivyo lakini huko nje twasifiwa. Hatusifiwi kwa ajili ya mbio tu, bali pia kwa uhodari wa uchumi, elimu, mipango na uongozi na siasa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa hakika, tumefika wakati ambao sisi lazima tuwaunge mkono na kuwasaidia wakulima. Najua wenzangu wamezungumza juu ya ukulima. Bila chakula huwa hakuna maendeleo. Chakula kwanza, ndipo uchumi uanze kukua. Kwa hivyo, lile suala la kuangalia bei ya mbolea ni suala muhimu sana. Pia, tuwaambie wananchi kokote waliko waanze ukulima hata katika sehemu ambazo kilimo hakiridhishi. Tuwe kitu kimoja. Tuungane sawa sawa. Tusonge mbele sawa sawa. Tuwe na sauti moja. Mkenya yeyote atakayehujumu mmoja wetu basi ni adui. Mara nyingine mimi husema: \"Kamata kamata, kamata adui\"."
}