GET /api/v0.1/hansard/entries/197182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 197182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/197182/?format=api",
"text_counter": 70,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Abuchiaba",
"speaker_title": "The Member for Lamu East",
"speaker": {
"id": 3,
"legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
"slug": "abu-chiaba"
},
"content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, jina langu ni Abu Mohammed Abuchiaba. Mimi ni Mbunge wa Lamu Mashariki katika Mkoa wa Pwani. Kwanza kabisa ninataka kumpongeza Spika wetu mpya, ambaye ametuongoza kwa miezi mitatu. Amekuwa na muongozo mwema, ukakamavu na imetambulika dunia nzima kwamba anastahili kuweko katika Kiti hicho. Pili, ninawashukuru watu wa Lamu Mashariki kwa kunichagua mara ya tatu ili niweze kuwahudumia vyema. Ni ahadi yangu ya kwamba nitawatendea yale ambayo ninaweza. Nitakuwa kiongozi ambaye analingana na matakwa yao. Bw. Naibu Spika wa Muda, Hotuba iliyotolewa na Rais Mwai Kibaki ilikuwa ya kusisimua. Pia ilikuwa na busara kubwa. Kwanza kabisa, vile nchi hii ilivyokuwa inaendelea kwa miezi mitatu baada ua Uchaguzi Mkuu, imeonekana kwamba Kenya ilikuwa inajulikana kama nchi ya amani, inayopenda watu na nchi ambayo haipendi ukabila. Inaonekana kwamba uchaguzi uliopita umeleta ukabila zaidi. Umeleta mafarakano na fitina nyingi ambavyo vimeishukisha hadhi ya Kenya. Marafiki wa Kenya dunia mzima walitukimbilia ili waiokoe nchi hii. Tuna wajibu mkubwa wa kuwashukuru viongozi wetu, Rais Mwai Kibaki na mhe. Raila kwa yale ambayo walifanya ili kuirudisha nchi hii katika hali yake ya zamani; kujulikana kama nchi ya amani. Isiwe tu eti Wakenya 1,200 walifariki tu, bali iwe ni kielelezo kwa viongozi wote walioko hapa. Tuwakumbuke na isiwe damu yao imemwagika bila sisi kuyatekeleza yale waliyopigania. Tunaweza kuyatekeleza hayo kwa kusimama imara na kuhakikisha kwamba haki ya mnyonge inatekelezwa. Haki ya mnyonge, Mswahili anasema, haiwezi kutekelezwa isipokuwa makabila makubwa yakitaka. Watu wa makabila makubwa ni lazima wakubali kwamba ndugu zao ambao hawakubahatika kutoka kwa makabila makubwa wana haki vile vile ya kuishi. Katika ugawaji wa sera za maendeleao, wao pia wanastahili kupata maendeleo pia. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningependa kugusia kidogo mambo yanayotukumba baada ya miaka 45. Watu wa sehemu ya Lamu hulilia barabara moja. Mwenyezi Mungu ametubariki na barabara hiyo moja. Viongozi waliopita wamezungumzia barabara ya Lamu mara nyingi ili barabara ya Lamu iweze kurekebishwa katika kipindi hiki. Viongozi wameamua wafanye ugawaji sambamba na haki. Mimi ni Mbunge wa Lamu Mashariki. Hili ni eneo la Uwakilishi Bungeni ambalo liko katika Bahari ya Hindi. Kutembea kwangu kule ili niweze kukamilisha sehemu ya Lamu Mashariki inategemea vile maji ya bahari yalivyo na kiasi kilichoko. Kuna hatari ya bahari na siwezi kukamilisha kutembea ila tu baada ya siku mbili. Watu huona ya kwamba sehemu ya Lamu Mashariki ikiwa ndogo, lakini shida zilizoko ni nyingi. Katika sehemu hiyo, maji ambayo Wakenya halisi hutumia, hutoka mbinguni. Ninajua jambo hili linawashangaza. Ni mpaka mvua inyeshe ili watu wa sehemu hiyo watie maji kwenye birika na kuyatumia hadi msimu mwingine wa mvua. Kwa hivyo, tunatarajia mipangilio ya ugawaji wa rasilmali iweze kuangalia mambo kama hayo. Bw. Naibu Spika wa Muda, mambo yaliyotokea ya ukosefu wa amani yameathiri sana sehemu za Mkoa wa Pwani. Watu wengi wamepoteza kazi, kwa sababu sehemu hizo wao hutilia maanani utalii. Watalii hawawezi kuja hapa wakisikia kwamba sehemu ya Burnt Forest inachomeka, hata ikiwa sehemu ya Lamu huko pwani ina amani. Vita hivyo huathiri maendeleo ya March 20, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 337 utalii. Kwa hivyo, tunatarajia ya kwamba viongozi wa Serikali ya Muungano wataleta mabadiliko ya kimsingi ili tuwe na ugawaji sawa wa sera katika sehemu zote za nchi. Kwa hayo machache, naunga mkono Hotuba ya Rais Mwai Kibaki."
}