HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 197288,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/197288/?format=api",
"text_counter": 26,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kambi",
"speaker_title": "The Member for Kaloleni",
"speaker": {
"id": 39,
"legal_name": "Samuel Kazungu Kambi",
"slug": "samuel-kambi"
},
"content": " Bw. Spika, asante sana kwa kuangaza macho yako yenye adili na kunitambua nizungumze katika Bunge hili. Nakushukuru sana kwa kuchaguliwa kwako kuwa Spika wetu. Ningependa pia kuwashukuru watu wa Kaloleni kwa kunipiga kura kwa wingi. Bw. Spika, nataka kujiunga na waheshimiwa Wabunge kupongeza Hotuba ya Rais. Nataka kuwashukuru watu wote waliohusika na mazungumzo ya kuleta amani hapa nchini wakati nchi yetu ilikuwaimeshika moto. Waliacha kazi zao ili watusaidie kutokana na janga hilo. Ninawaombea maisha marefu. Bw. Spika, kwa wale ambao hawanijui, mimi ni Mbunge wa Kaloleni. Eneo hili la Kaloleni ndilo masikini zaidi hapa nchini. Kulinga na historia, elimu ilianza kule Kaloleni wakati wa mkoloni. Masikitiko makubwa ni kamba watu wa Kaloleni ni masikini sana na wengi wao hawajasoma. Bw. Spika, tuna shida nyingi katika nchi yetu. Tunamshukuru Mungu vile tulikuja pamoja na kutambua Kenya ni kubwa kushinda sisi wenyewe. Ningependa kuwashukuru wahusika wakuu; Rais Mwai Kibaki na mhe. Raila Odinga, ambaye ni Waziri Mkuu mtarajiwa. Walisikia kilio cha Wakenya na wakaona kweli ni lazima waje pamoja. Hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana bila sisi kushikana pamoja. Waswahili husema hivi: \"Hata ukiwa una nguvu namna gani lakini ukiwa pekee yako huwezi ukamchinja ng'ombe au mbuzi\". Kwa hivyo, vile walivyofanya wahusika wakuu hawa ilikuwa ni kitendo ambacho hakijawahi kufanyika katika historia ya Kenya. Ninawapongeza na kuwasihi waendelee na moyo huo huo. Kenya itaendelea. Bw. Spika, Hotuba ya Rais iligusia mambo mengi. Jambo ambalo lilizungumzia zaidi ni kuhusu ukabila. Tusipojihadhari na ukabila utaangamiza nchi hii. Umekuwa ni kidonda sugu tangu tupate Uhuru. Wakati umefika sasa wa sisi kuupiga vita ukabila hapa nchini. Nchi hii inawezakupiga hatua za kimaendeleo ikiwa tutaupiga vita ukabila hapa nchi. Wakati umefika wa sisi kuwakaribisha watu wetu popote wanapozuru. Haifai kuwauliza watokako. Wakaribisheni kama ndugu. Haina haja kumuuliza ndugu yako anakotoka au wewe ni mtu wa wapi? Ningeomba tuuzike ukabila katika kaburi la sahau. Tunaweza kufanya hivyo kwa kuwasilisha miswada hapa Bungeni ya kuwalazimisha watu wetu kuoa kutoka kabila tofauti. Hii ndio njia mwafaka ya kuupiga vita ukabila. Ni aibu kuona ya kwamba nafazi za kazi hupatikana kwa misingi ya kikabila. Tukifanya hivyo, tutakuwa tumegawanyika kwa misingi ya kikabila. Bw. Spika, shida ambayo ilitokea juzi haikusababishwa na unganyifu wa kura, bali ni kwa sababu ya kutokuwa na usawa wa rasilmali zetu. Kuna makabila mengine ambayo hayajaendelea, kwa mfano, Wagiriama. Kwa hivyo, ningependa kuona usawa katika kila pembe na hasa hapa Bungeni. Ningependa kuona usawa wa raslimali, elimu, kilimo na mambo mengine mengi. Juzi tuliona ugavi wa mamlaka baina ya viongozi sugu wetu. Basi tugawanye mambo yote. Tuwe watu 276 PARLIAMENTARY DEBATES March 19, 2008 adili na tutekeleze haki baina yetu. Bwana Spika, suala lingine ambalo linatatiza ni la uajiri. Tungeomba vile vile nafasi za kazi ziweze kugawanywa sawa sawa. Katika Hotuba yake, Rais aliongea juu ya utalii. Juzi, Dubai ilikuwa jangwa, lakini ukienda huko leo, utaona ya kuwa wanapokea watalii zaidi ya 30 milioni kwa mwaka. Hapa nchini hutajafikisha hata watalii moja milioni. Kwa hivyo, tunatakiwa kutunga Miswada ambayo itawavutia watalii wengi kuja humu nchini. Pia, tunatakiwa kuangalia mbinu zingine ambazo zitaimairisha uchumi wetu. Bw. Naibu Spika, watu wa Kaloleni wanakumbwa na ukosefu wa maji. Kuna mzungu mmoja ambaye alisema maji ni uhai, lakini utashangaa ukiona jinsi watu wa Kaloleni wanaishi bila maji safi. Watu wa Kaloleni wanatumia maji machafu ambayo hawezi kutumiwa hata na mifugo. Ningeomba Bunge hili na Wizara inayohusika kuhakikisha kwamba watu wa Kaloleni wanapatiwa maji. Ukiangalia nchi kama Israeli, utaona ya kuwa ilikuwa jangwa lakini wanakuza vyakula ambavyo wanauza katika nchi za nje. Mashamba yetu yana rotuba, kwa nini hatuwezi kujifunza kutoka kwa Israeli ili Kenya iweze kuendelea? Tuna rasilmali nyingi lakini hatujui kuzitumia. Ukiangalia ukulima wetu, utaona kwamba bei za mbolea imepandishwa mara kumi. Mkulima wa kawaida hawezi kununua mbolea. Ningeomba Serikali, haswa tukitarajia mvua kunyesha kwa msimu huu, ipunguze bei za mbolea ili wakulima waweze kupata mazao mazuri. Bwana Spika, sitakuwa nimefanya vizuri ikiwa nitamaliza kuzungumza bila kugusia swala la elimu. Elimu ndio msingi wa maisha. Tunashukuru tuna elimu ya bure, lakini bado haijaimarishwa sawa sawa. Tungeomba Bunge hili liweke sheria ambayo itawezesha elimu ya bure kutolewa katika kila sehemu ya nchi yetu. Sitaki nitembee Turkana na kuwaona Waturkana hawajaenda shule. Tunapenda kuwa na usawa katika elimu. Kwa kumalizia, tungeomba Serikali ihakikishe kwamba shida ambayo imetokea haitatokea tena. Hatukutarajia kuwa shida hii itatokea katika nchi yetu. Hata kama tulikuwa na shida mbali mbali tangu wakati wa ukoloni, hali hii ilitokea kwa sababu ya uchochezi. Kwa hivyo, ninaomba tusiishi na chuki. Tuishi kama ndugu na dada au baba na mama. Tusiishi tukisema huyu ni Mjaluo, Mkikuyu au Mgiriama. Tunaomba tuangamize ukabila. Ninakushukuru, Bwana Spika, kwa kuchaguliwa. Vile vile, ninawashukuru wenzangu kwa kuchaguliwa. Kampeni ilikuwa ngumu. Kwa hivyo, ninaomba tuungane mkono kwa sababu ni katika muungano wetu ambapo tutaendelea; haswa tuangalie swala la Mkoa wa Pwani. Asili mia sitini ya uchumi wa Kenya unatoka Pwani, lakini barabara katika Mkoa wa Pwani ni mbaya zaidi. Kwa hivyo, tunaomba Wizara inayohusika iangalie suala la mabaraza kule Pwani. Hii ni kwa sababu huko ndiko tuna Bandari ambayo inatumiwa na nchi jirani ambazo hazina Bandari. Kwa hivyo, barabara zikiwa mbaya, usafiri utakuwa ghali sana. Bwana Spika, ninakushukuru kuwa kunipa wakati huu. Mungu akubariki."
}