HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 197726,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/197726/?format=api",
"text_counter": 53,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Ahsante sana Bw. Spika. Ningependa kuanza kwa kutoa shukrani kwa wananchi wapendwa wa Taveta walioamua kunipa muhula wa pili na kupiga kura kisawasawa wakati wa uchaguzi mkuu. Pia ningependa kutoa pongezi kwa akina mama; kwanza, wale 15 ambao walichaguliwa kuja katika Bunge hili la Kumi. Ningependa kuwapongeza kwa sababu wameanza kazi yao kwa imani na upendo kwa watu wao. Wakati Wakenya walikuwa wakitatizika, akina mama hao walikimbia kwenda kwenye mawakilisho yao ili kuzungumza na wale ambao waliwatuma huku Bungeni. Natamani akina mama wangekuwa wengi zaidi humu Bungeni. Si ajabu Kenya isingekuwa na matatizo makubwa tuliyonayo. Ningependa kuwatolea shukrani Rais Kibaki na mhe. Raila kwa kutia sahihi mkataba ambao utatutoa kwenye matatizo ya kisiasa ambayo yametukumba tangu wakati tulipopiga kura. Katika Hotuba ya Rais, alitaja kwamba kuna masuala fulani ambayo ni lazima yatendeke ili Kenya iweze kusonga mbele. Ningependa kumuunga mkono kwenye masuala yote aliyoyataja. Bw. Spika, Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano ni muhimu sana. Tuliwaona wakuu wa dini mbali mbali wakikiri kuwa wao pia walipendelea pande fulani za siasa. Badala ya kuwaeleza watu wachague viongozi waliotaka kuchagua, wao pia walijifanya kama wanasiasa. Kuna Wabunge 222 hapa. Sisi Wabunge pia tulipita kila kona ya nchi hii tukiwaeleza watu umuhimu wa kutupigia kura kwa sababu sisi ni wakabila lao. Kwa hivyo, hata sisi tuna jukumu la kusimama na kusema ukweli kabla Tume hii haijaanza kazi. Tukubali kwamba tumewakosea Wakenya na tuliwadanganya kwa misingi ya kikabila ili tuweze kuja Bungeni. Si sawa kwa Wakenya kudanganywa namna hiyo. Kamwe, Wakenya wasikubali kudanganywa namna hiyo wakati tunapoingia ukurasa mpya wa nchi hii yetu ya Kenya tunayoipenda. Hii ni nchi ambayo ilikuwa na msingi imara, lakini sisi wanasiasa tuliamuwa kuiharibu. Kweli Kenya ni kubwa. Si rahisi Kenya kutikisika. Kwa hivyo, sisi wanasiasa tuliitia nchi hii hasara kubwa. Bila sisi kukubali kuwa tuna makosa, itakuwa shida kwetu kuzungumza na watu wetu kule mashinani na kuwaomba wakae pamoja huku sisi tukiwa bado tunawawekea finyo kichinichini bila kukubali matatizo tuliyonayo. Kwa hivyo, ningependa kuwaomba Wabunge wenzangu kutoka kila chama, alivyosema Rais Kibaki, twende sote kuwatembelea watu mashinani. Nafikiria hilo ndilo jambo muhimu zaidi. Ningependa kumpongeza Rais Kibaki kwa kuzungumzia kinaganaga juu ya matatizo yaliyotukumbuka na jinsi Kenya hii itaingia kwenye ukurusa mpya tukiwa pamoja na kufanya kazi kama Wakenya walio kitu kimoja. Kwenye Hotuba yake, alizungumza juu ya chemchemi ya Mzima ambayo imekuwa ikitoa maji upande wa Pwani ya chini. Chemchemi hii imetoa maji kwa muda mrefu tangu karne 154 PARLIAMENTARY DEBATES March 13, 2008 iliyopita, lakini haijatumika kikamilifu. Rais Kibaki alitaja kwamba mradi huu ni muhimu sana na sharti ukamilishwe ili maji yaweze kuwafikia watu katika Mkoa wa Pwani wote. Bw. Spika, ningependa kuzungumzia juu ya utalii. Sisi viongozi tunafahamu kwamba pwani ya nchi yetu ndiyo inashikilia masuala ya utalii katika Kenya nzima. Lakini sisi wanasiasa tulienda Mkoa wa Pwani na kueneza habari za chuki ambazo ziliwafanya vijana waanze kuvurugana. Basi tuliwatisha watalii na wakakosa kuja kwetu. Nawaombea wale waliokuwa mstari wa mbele kuharibu utali katika nchi hii wapatiwe fursa ya kuwa Mawaziri katika Wizara ya Utalii ili waweze kurekebisha matatizo waliyotuletea. Bw. Spika, njia bora ya kuuza utalii hapa Kenya inahitaji sote tuungane pamoja ili tujenge nchi yetu tukijua kuwa utalii ni kitega-uchumi muhimu katika nchi yetu. Vile vile, ningependa kuzungumza juu ya matatizo yaliyowakumba wale wapendwa Wakenya waliofurushwa kutoka kwenye makao yao ya miaka mingi. Ukifika kwenye zile kambi wanakoishi Wakenya wenzetu, utabubujikwa na machozi kwa urahisi. Akina mama, watoto na watu wakongwe wanapata mateso makubwa - si kwa sababu sisi katika Serikali hatuwezi kuwasaidia. Ukweli ni kwamba, Wakenya hawafai kuishi kwenye kambi. Wakenya hao wanateseka sana kwa sababu ya kuishi kwenye kambi. Ningependa kuwahusisha Wabunge wenzangu wote. Nawaomba tutetembelee kambi hizo ili tuelewe matatizo yaliyowakabili watu wetu baada ya sisi kuzungumza mambo yaliyoleta chuki katika nchi yetu. Serikali inafahamu kuwa watu waliofurushwa kutoka makwao wameishi katika maeneo fulani fulani kwa muda mrefu. Wengine wamezaliwa huko na hawana kwingine watakakokuita kwao. Kuna umuhimu kwetu sisi kung'ang'ana na kuhakikisha kwamba kila mtu amepata haki yake. Hatutakuwa tunasema kuwa tunataka kusonga mbele ilhali sisi kisiasa tumechanganyikiwa. Sharti tuwe kitu kimoja la sivyo, wananchi wataendelea kuteseka. Nawaomba Wabunge wenzangu tushikane pamoja kama alivyosema Rais Kibaki. Alisemba kwamba tuende tukawazungumzie watu ili waweze kutulia katika makao yao. Bw. Spika, si kweli kwamba kuna matatizo sugu ya kihistoria. Si kote. Kwingi kuliko na matatizo ni kule ambako wananchi walikuwa wametokwa jasho wakajinunulia maeneo. Ilikuwa ni haki yao kuwa pale kwa sababu walinunua na akajenga pale. Lakini sisi wanasiasa tunapenda kusimama hadharani kila siku na kusema kuwa haya ni matatizo ya kihistoria. Historia gani ipo mahali ambapo mwananchi ameenda kujichukulia mkopo na akajinunulia eneo kisha akajenga? Hilo ndilo swali ambalo ningependa kuwauliza wenzangu ili walifikirie. Hii ni kwa sababu tunapenda sana kurudia hayo masuala ambayo, kusema ukweli wa Mungu, si mambo ya kweli. Wengi wao, hata sasa hivi, wakiwa kwenye kambi wanatulilia wakituuliza, \"Je, tutalipa mikopo yetu vipi?\" Hilo ndilo swali ambalo naulizwa. Kwa hivyo Bw. Spika, nawaomba Wabunge wenzangu, hata kama katika wakilisho lako hakuna shida--- Katika yale mawakilisho ambayo yana shida, naomba tutembee pamoja ili tusikize vilio vya Wakenya. Tusaidiane ili tufanye uamuzi. Kuna kamati iliyoundwa katika Wizara yangu. Kamati hiyo ina makatibu wa kudumu kutoka Wizara saba. Vile vile, mimi mwenyewe niliona umuhimu wa kuwaalika wenzangu kutoka upande wa Chungwa kuwa katika kamati hiyo ili tuweze kufanya uamuzi pamoja kuhusu wapendwa wetu."
}