GET /api/v0.1/hansard/entries/197728/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 197728,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/197728/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Kamati hiyo imefanya kazi. Lakini kazi yenyewe ni jukumu kubwa na tunahitaji kushikana mikono pamoja. Tunapoenda kwenye awamu ya pili ya kuhakikisha kuwa hawa waliofurushwa kutoka kwenye makao yao wanapata makao mapya, tusizungumze tu na kusisitiza kuwa masuala hayo lazima yatekelezwe kwa muda fulani. Hii ni kwa sababu si rahisi kufanya hivyo. Ikiwa kazi haitafanywa vizuri, utagundua kwamba hata wale ambao sio waathirika ndio watafaidika kuliko wale ambao waliathirika. Kwa hivyo mtuwie radhi kwa sababu tunang'ang'ana tunavyoweza. March 13, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 155 Serikali ina jukumu la kuhakikisha kwamba wale ambao wako katika kambi hizi wamepata makao yao, wametulia, na waweze kuendelea na hali yao ya maisha ili nao pia wapate matunda kama Wakenya wengine. Matunda siyo ya Wabunge peke yao, bali ni ya Wakenya wote; hasa wale ambao wametupatia fursa ya kuja kwenye jumba hili la kifahari. Bw. Spika, nikimalizia, hivi maajuzi, tulikuwa na uchaguzi wa Mameya. Kulikuwa na fujo na vurumai kila mahali kwa sababu kila mtu alikuwa na pilkapilka hizo. Nashukuru kwa vile Mhe. Rais ametuhimizaa tuwe na sheria ya Mameya kuchaguliwa kutoka mashinani, ili pilkapilka hizo zipungue. Kenya ni yetu na ningependa kumalizia kuwa, kama vile Mhe. Rais alivyosema, kuwa tunahitaji amani. Nataka kuwakumbusha wenzangu kwamba amani haiwezi kubadilishwa na chombo chochote kile. Amani ni haki yetu. Lakini kuna umuhimu wa sisi kuchukulia amani kama jambo la muhimu zaidi. Inafaa sote tuwe katika mstari wa mbele kudumisha amani. Ahsante sana!"
}