GET /api/v0.1/hansard/entries/199447/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 199447,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/199447/?format=api",
    "text_counter": 442,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Capt. Nakitare",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ili niunge mkono Hoja hii kuhusu sera ya vijana. Shida za vijana zinatokana na mpango mbaya ambao ulikuweko kuanzia zamani. Mambo haya hayakuanza mwaka huu au miaka miwili au mitatu iliyopita. Ukiangazia jamii kama ya kutoka Bara Asia, mtoto akihitimu umri wa kusoma, baba yake anamfunza hesabu ya biashara. Hivyo, basi, mtoto huyo anakua akiwa anajua hesabu inayohusu biashara. Leo tumeleta Sera ya kutenga pesa zitakazopewa vijana ili wajimudu. Je, tunawafundisha vijana wetu kuvua samaki ama tunawapatia samaki? Ikiwa tunataka kuwafundisha wajue kuvua samaki, ni lazima wajue urefu wa ndoano na mahali pa kutafuta samaki hao. Nashangaa kwamba Sera hii ambayo Waziri ameleta inahusu watu ambao wamesoma. Ni lazima turekebisha swala hili. Ni miaka mingi sasa tangu hayati Mzee Kenyatta alimtuma marehemu J.M. Kariuki kwenda Cuba. Aliporudi, alianzisha chuo cha Vijana wa Huduma ya Taifa, yaani, National Youth Service. Madhumuni ya kuanzisha chuo cha National Youth Service ilikuwa ni kuwafundisha vijana ambao hawakuwa shuleni na wale ambao wangelielewa ufundi ili waweze kujitegemea kimaisha. Ningependekeza kwamba Wizara hii ingewalazimisha vijana ambao ni asilimia 65 ya watu wote wa Kenya wajiunge na National Youth Service. Pesa nyingi zinafaa kutumia katika vyuo vya National Youth Service ili kuwafundisha. Wakitoka huko, watakuwa wamekomaa kiakili. Hivyo, basi, wakipewa nafasi ya kufanya biashara ama ufundi wataifanya bila wasiwasi. Siku hizi tunatafuta wanakandarasi wa kukarabati barabara. Miaka iliyopita National Youth Service ilikuwa inajenga barabara. Kwa mfano, ilijenga barabara ya kwenda Garissa. Ni vijana ambao hawakuwa na shahada za digrii lakini ni watu ambao walikuwa wemefundishwa sanaa mbali mbali na kuendesha tingatinga. Je, kuhusu hizi pesa ambazo vijana wanapewa kupitia hazina ya kuwaendeleza vijana, kuna mtu yeyote ambaye amefanya hesabu na kusema kwa mfano: \"Nikikupa Kshs50,000 za kufanyia biashara, utapata faida kiasi fulani?\" Je, tumewaelimisha vijana kuhusu faida na hasara katika biashara au tunawafurahisha kwa kuwapa pesa tu? Tumewapatia mawazo lakini tumewapatia pia tamaa. Hivyo basi wasipotengewa pesa katika Bajeti ya mwaka ujao, watailazimisha Serikali kuwapa pesa. Wataiuliza Serikali: \"Kwa nini leo hatujapewa pesa ilhali mlitupatia mwaka uliopita?\" Na itakuwa ni lazima kwa Serikali kujiandaa kwa mambo hayo. Kwa hivyo, mimi naona ni mpango mzuri. Wale vijana wengi ambao wamewacha shule na ambao wamehitimu umri wa miaka 18 wasukumwe National Youth Service (NYS). Waende wafanye kazi huko. Wawe na mafunzo ya miezi 18 na wakitoka huko, watakuwa wamekomaa. Kwa hayo machache, Bw. Naibu Spika, naunga mkono."
}