GET /api/v0.1/hansard/entries/201267/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 201267,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/201267/?format=api",
"text_counter": 303,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Wamwere",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Information and Communications",
"speaker": {
"id": 352,
"legal_name": "Koigi Wamwere",
"slug": "koigi-wamwere"
},
"content": " Bw. Naibu Mwenyekiti wa Muda, nataka kukariri yaliosemwa, kwamba wafisadi hawaonyeshi wazi wanakoweka mali yao. Kila wakati, wafisadi huficha mali yao pahali popote wanapoweza kuyaficha. Kama huwezi kufichua kule kulikofichwa mali na wafisadi, usijidanganye kwamba unapigana na ufisadi. Katika nchi hii, tunajua ya kwamba mali yaliyoibiwa kifisadi yamefichwa katika benki za nchi za nje. Watu wameweka mali yao katika majina ya ndugu zao, marafiki zao, wake zao na watu wengine. Kwa hivyo, kupendekeza hapa kwamba mtu asifuatwe hadi kule alipoficha mali ya wizi ni kama kusema kwamba Bunge hili limeamua kuunga mkono ufisadi na wafisadi. Siku moja, Bunge hili litakuja kulaaniwa kwa jambo hili linalolifanya leo!"
}