GET /api/v0.1/hansard/entries/204253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 204253,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/204253/?format=api",
    "text_counter": 177,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wario",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Ministry of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, rai walizotoa waheshimiwa Bw. Muturi na Bi. Njoki Ndung'u ni nzuri na za ukweli. Hata hivyo, rai zao zinahitaji Hoja nyingine, siyo hii. Hoja hii itakuwa sumu kwa nchi hii. Ni Hoja mbaya inayostahili kupingwa na kila mheshimiwa Mbunge aliye ndani ya Bunge hili. Bw. Naibu Spika wa Muda, yapasa tujiulize ni kwa nini Hoja hii imeletwa Bungeni leo. Hoja hii imeletwa leo kwa sababu miezi michache ijayo, tutaenda kupiga kura. Nia ya Hoja hii ni kuamsha hisia za kikabila na chuki na uhasama baina ya Wakenya!"
}