GET /api/v0.1/hansard/entries/204268/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 204268,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/204268/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wario",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Ministry of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, tulinyamaza wenzetu kutoka Upinzani walipokuwa wakichangia Hoja hii. Wao pia yafaa watuvumilie sasa kwa sababu ni lazima wasikie rai zetu. Si lazima tuichukue Hoja jinsi inavyoletwa kwetu. Sisi tuko hapa kuchambua. Bw. Naibu Spika wa Muda, ningewaomba wenzetu waangalie nyuma. Tuliambiwa hapa kwamba Wizara zenye fedha nyingi zimepewa Wakikuyu. Je, kabla Wizara hizo kupewa Wakikuyu, zilikuwa chini ya Mawaziri gani? Kwa mfano, Wizara ya Kawi ilikuwa na Waziri yupi? Je, Wizara ya Barabara na Ujenzi ilikuwa chini ya nani? Swali ambalo ningependa kuwauliza ni hili: Wizara ya Elimu inaongozwa na mhe. Prof. Saitoti. Je, elimu ya bure imekatazwa katika Mkoa wa Nyanza? Haijakatazwa! Tuangalie ni nini ambacho amefanya ama ni mambo gani ambayo ametekeleza. Tusichunguze ni nani kutoka kabila gani yuko katika Wizara gani. Sera ya elimu ya bure imetekelezwa. Je, sera hiyo imewafaidi Wakenya wote ama inawafaidi wenzetu kutoka Mkoa wa Kati peke yao? Sharti tuangalie ni nini Wizara hiyo imetekeleza."
}