GET /api/v0.1/hansard/entries/204278/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 204278,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/204278/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Wario",
    "speaker_title": "The Assistant Minister, Ministry of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, nikimalizia mchango wangu, ningependa kusema mambo mawili. Kwanza, tusiwe na mazoea ya kusema eti Kenya ina makabila 40. Kuna makabila mengi ambayo hayajasajiliwa. Kwa hivyo ile hesabu ya kusema kwamba Kenya ina makabila 42 ni ya kikoloni. Leo, hapa Kenya kuna makabila mengi ambayo hayajatambulika. Unaweza kuongeza katika makabila hayo Mmarakwet na Mnyayaya. Kuna makabila zaidi ya 50 humu nchini! Mwisho, Bw. Naibu Spika wa Muda, sharti tuingalie Kenya kama Kenya wala siyo kama nyumba ya ukabila. Tukipitisha hii Hoja kuwa sheria, italeta mizozo, chuki na uhasama katika nchi hii. Tuitupe haraka iwezekanavyo! Ninapinga Hoja hii."
}