GET /api/v0.1/hansard/entries/204921/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 204921,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/204921/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwandawiro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 253,
        "legal_name": "Mwandawiro JD Mghanga",
        "slug": "mwandawiro-mghanga"
    },
    "content": "Bw. Spika, kuna madai kwamba katika Mkoa wa Kati na mitaa ya mabanda hapa Nairobi, vijana wengi wanaishi kwa hofu sana. Wanahofia kukamatwa na kufungwa na hata kuuawa na polisi wakati wowote ule. Hata kuna madai kwamba vijana wengi wanatoroka kutoka sehemu za Mkoa wa Kati na kwenda pahali pengine. Je, Waziri Msaidizi anaweza kuhakikishia Bunge hili kwamba hakuna ugandamizaji wa vijana na wananchi kwa jumla katika Mkoa wa Kati na mitaa ya mabanda huku Nairobi kwa kuwasingizia kuwa na uhusiano na kundi haramu la Mungiki ?"
}