HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 205415,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/205415/?format=api",
"text_counter": 141,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwaboza",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Immigration and Registration of Persons",
"speaker": {
"id": 243,
"legal_name": "Anania Mwasambu Mwaboza",
"slug": "anania-mwaboza"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii ili nami nichangie Hoja hii ya makadirio ya matumizi ya fedha katika Wizara ya Uchukuzi. Kwanza ningependa kuitolea Wizara hii heko kwa jinsi inavyojitahidi katika masuala ya uchukuzi. Mbali na hilo, kuna suala la Shirika la Kenya Airways ambalo linaendelea kufanya vizuri nchini. Hata hivyo, kama walivyosema waheshimiwa Wabunge wenzangu waliozungumza hapa, kuna taabu za hapa na pale katika shirika hilo lakini malumbano hayakosekani katika kila shughuli. Katika Kenya ya leo, Wizara hii ingefikiria kubuni \"Kenya Sea Airways\". Kwa nini nimesema hivyo? Ni kwa sababu Serikali yetu iliahidi kuzalisha kazi kwa vijana ambao ni wengi humu nchini. Nyanja hii bado haijafikiriwa kabisa. Kwa mfano, kule Tanzania, watu husafiri kutoka Dar-es-Salaam hadi Zanzibar wakitumia ile sehemu ya maji iunganishayo kisiwa cha Zanzibar na Dar-es-salaam. Mambo kama haya yanazalisha ushuru kwa taifa. Vile vile yanatoa fursa ya uzalishaji wa kazi na kutoa utajiri kwa wale ambao watakuwa katika himaya hii ya ufanyaji kazi. Katika nchi ya Kenya, kilomita zaidi ya 640 za mwambao wa pwani zimeachwa wazi bila kuwepo na biashara zozote. Wakati umefika kwa Wizara hii kufikiria ikiwa mambo 3704 PARLIAMENTARY DEBATES September 5, 2007 kama haya yanafanyika katika nchi nyingine. Kama Wizara hii ingetengeneza sea ways, basi watu wataweza kusafiri hadi jijini Mombasa, Lunga Lunga, Kilifi, Malindi hadi Lamu. Shughuli hii ingezalisha kazi nyingi ambazo zingezidi zile kazi nusu milioni Wakenya waliahidiwa. Vile vile shughuli hii ingepunguza misongamano iliyoko katika barabara zetu ambazo kwa mara nyingi uzito wa mizigo na magari makubwa yanafanya barabara kuharibika. Kwa hivyo, wale ambao ni watungaji sera katika Wizara hii, wana jukumu kubwa kuhakikisha kwamba tunaendesha Kenya mbele katika nyanja hii. Bw. Naibu Spika wa Muda, kitu kingine cha pili muhimu ambacho ningependa kuzungumzia kuhusu Jiji la Mombasa ni kwamba kuna feri ya kwenda Likoni na daraja moja la kuelekea Mombasa Kaskazini, upande wa Nyali. Kule Dubai kuna usafiri wa baharini kupitia njia ya feri. Wamejenga pantoni ambazo huwezesha meli fulani kuvukisha watu kwa bei ya chini. Kwa njia hii, wanazalisha kazi. Kwa mfano, kutoka Mkomani English Point kufika Port Jesus, tungekuwa na usafiri wa baharini. Magari yanayopitia kwenye ile daraja yangepungua. Mizigo ingepitishwa kwa thamani ndogo na ingepunguza bei ya uchukuzi wa matatu ambayo kwa sasa yanawadhulumu watu wetu. Utaona ya kwamba mahali pa Kshs10, watu wetu wanalipa Kshs30. Hizi ni fikira ambazo zizafaa kuzingatiwa ili jiji la Mombasa lipatiwe hadhi yake. Hata abiria wanaosafiri wataweza kujimudu ikiwa mzigo huu wa usafiri utakuwa umepunguzwa. Bw. Naibu Spika wa Muda, suala lingine muhimu la kuzungumzia ni jinsi magari yanavyofanya ajali katika barabara zetu. Shida hii inatokea kwa sababu Wizara ya Uchukuzi ndio inayoshughulika na sheria za barabarani. Lakini ni nani anayefaa kutekeleza jukumu hili? Utakuta ni maofisa wa idara ya trafiki. Hata hivyo, hawa maofisa hawako chini ya Wizara ya Uchukuzi. Kama hakuna ushirikiano na idara hii, basi itakuwa vigumu kwa Wizara kutekeleza jukumu lake. Maombi yangu ni kwamba Ofisi ya Rais ishirikiane na Wizara ya Uchukuzi ili tupunguze ajali barabarani. Kwa mfano, tunaweza kuwa na askari maalum chini ya Wizara ya Uchukuzi ili watekeleze sheria hizi. Hii inawezekana kwa sababu Shirika la Reli lina Railway Police. Pia shirika la Bandari ya Mombasa lina Port Police. Kwa nini hatuwezi kuwa na hawa askari chini ya Wizara hii ili watekeleze sheria za trafiki? Mara nyingi, kumekuwa na mvutano kati ya Wizara hizi mbili. Mmoja anamlimbikizia mwingine matatizo. Kumekuwa na hali ya vuta nikuvute na huku watu wetu wanapoteza maisha yao kutokana na ajali barabarani. Bw. Naibu Spika wa Muda, suala lingine muhimu la kuzungumuzia ni kazi ya mabaharia. Miaka ya 1965, 1970 na 1980, vijana wengi walikuwa wakiajiriwa kazi kama mabaharia. Walikuwa wakisafiri kwa meli na kwenda ng'ambo kufanya kazi hiyo. Hivi sasa kumetokea sheria mpya ya kimataifa. Kila kijana ambaye anataka kwenda kufanya kazi kama baharia ni lazima awe na cheti cha STCW. Inahitajika mtu awe na discharge book na pasipoti ili aajiriwe. Kufikia sasa, nchi ya Kenya haijaweza kutoa vyeti hivo kwa sababu ya upungufu wa sheria fulani ambazo bado hazijapitishwa. Katika nchi jirani kama Tanzania wamepitisha sheria hizo. Vijana wetu ni lazima waende kule Dar-es-Salaam na kulipa Kshs30,000. Tuko na Chuo cha Bandari ambacho kinaweza kufanya mambo haya yote. Wakati umefika, Katibu na wenzake ambao wanatunga sera, wafikirie mambo haya. Hii inaweza kuzalisha nafasi za kazi zaidi ya laki moja kwa mwaka katika nchi hii. Serikali ya Thailand hupata utajiri wake kutokana na nyanja hii. Kwa hivyo, ni lazima fikira zetu Wakenya ziwe pana. Tukifanya hivyo, tutaweza kuendesha taifa letu vizuri. Bw. Naibu Spika wa Muda, suala lingine ambalo nitalizungumuzia, na ambalo mhe. Zaddock ameligusia, ni la Kenya National Shipping Line (KNSL). Nikifungua macho kulikuwa na meli mbili ambazo zilinunuliwa na ushuru wa nchi ya Kenya zikiwa chini ya KNSL. Meli hizi zimepotea kiajabu. Mpaka leo haijulikani ni nani aliziuza. Hakuna mtu yeyote anayezifuatilia. Hii ni himaya mpya ya utawala ambapo wangefuatilia mambo haya ili tujue ni nani alifanya udhalimu kama huu kusudi iwe kielelezo kwa wengineo ambao watakuja baadaye. Ni lazima tulinde September 5, 2007 PARLIAMENTARY DEBATES 3705 rasilimali ya mwananchi wa kawaida. Bw. Naibu Spika wa Muda, suala lingine muhimu ni kuhusu ubinafsishaji wa vituo vya mwisho au terminals za Kenya Ports Authority (KPA). Kwa mfano, kuna mwekezaji mmoja kwa jina Boss Freight. Amepatiwa vituo hivi aviendeshe kama mtu binafsi. Kuna hatari ya silaha kupitishwa ikiwa vituo hivi vitasimamiwa na watu binafsi. Pia kuna hatari ya madawa ya kulevya kupitishwa ikiwa yeye ndiye atakuwa anashika doria. Atakuwa na mamlaka na itakuwa ni vigumu kwa wakuu wa forodha, ama polisi wakawaida, kufanya uchunguzi katika sehemu hizo. Vile ninavyojua, katika sheria ya Kenya Airports Authority Act, vituo hivi ni mali ya wananchi. Mambo yale kama yalifanyika, wakati huu ni wa kufanya mabadiliko ili mambo haya yasifanyike tena. Kuna msongamano wa shehena katika bandari yetu kwa sababu ya madhambi yetu. Sehemu fulani zilibinafsishwa na kuuzwa. Huu ni wakati wa kurebisha matatizo haya. Bw. Naibu Spika wa Muda, suala lingine muhimu ni kupanua viwanja vya ndege kama kile cha Malindi. Kuna haja ya kupanua viwanja hivi. Ni wajibu wetu kuyapatia kipa umbele mambo kama haya. Tufanye ufunguzi wa sehemu zile ndio watalii wengi waweze kuja na mahoteli yetu yaweze kufaidika. Hatimaye, kazi itazalishwa na ile miji kuinuka. Bw. Naibu Spika wa Muda, suala lingine linalojitokeza ni kwamba, kumekuwa na mvutano baina ya baraza na bandari ya Kenya kuhusu ushuru ambao Baraza la Manispaa ya Mombasa lingetaka lipatiwe. Kumekuwa migogoro ya kesi. Ikiwa linafanyika katika nchi zingine, kuna umuhimu wa Bandari ya Mombasa kupata kiasi fulani cha ushuru ili litekeleze jukumu lake; kama vile kukarabati barabara ambazo zinaharibiwa na malori makubwa. Manispaa ya Mombasa haina fedha. Ikiwa ushuru huu utatolewa, basi itakuwa rahisi kwao kutekeleza wajibu wao kwa watu wa Mombasa. Mambo mengine ni haya ya usafiri kwa shirika la Kenya Airways. Mara nyingi tunakwama na kucheleweshwa. Unalipia ndege ya saa kumi na mbili na nusu. Unaambiwa itakuja lakini inachanganywa na ndege nyingine inayotoka nchi ya kigeni. Watu wanaosafiri na ndege mara nyingi ni wafanya biashara. Kwao, wakati ni kitu muhimu kuliko hata pesa. Ningependekeza kwamba yule mkurugenzi na Wizara ya Uchukuzi kwa jumla, wakaa na kuangalia iangalie matatizo haya yanaweza kutatuliwa kwa namna gani. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}